Sunday, May 3, 2020

๐Ÿ ๐Ÿฌ FURSA YA UFUGAJI BORA WA SAMAKI๐Ÿฌ๐Ÿฌ

Ufugaji wa Samaki kwenye Mabwawa


๐ŸŸDondoo hii tunazidi kufahamishana fursa zinazotuzunguka,ambazo kwa  uthubutu wa  mtu yeyote anaweza pata mafanikio makubwa

๐Ÿ Kutokana mahitaji ya samaki duniani kuzidi kushamiri  kwa sababu ya ongezeko la wingi wa watu na uhaba wa sehemu zenye maji ya asili kama mito na maziwa kwa samaki wa maji baridi pia bahari kwa samaki wa maji chumvi,kumezidi kuhamasisha watu kungundua namna za kuweza kujipatia kitoweo hichi haswa ikichochewa na hamasa inayotokana na faida ya nyama  nyeupe ya samaki katika mwili na afya ya binadamu.

๐ŸŸ๐ŸŸ๐ŸŸ๐ŸŸ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ
Katika kuiangalia fursa hii tutaangalia vipengele ambavyo kwa kufatilia wataalamu na wafugaji mbali mbali tumegundua vitasaidia sana kutoa mwanga kwenye fursa hii na kuzidi kutoa hamasa si ya kusoma tu makala mbali mbali ya ujasiriamali na tafiti za biashara bali pia kuchukua hatua stahiki katika kufanikisha malengo yako.


Vipengele hivyo ni:

  • Eneo,
  • Maji
  • Aina za mabwawa,
  • Ujenzi wa Bwawa,
  • Mifumo ya ufugaji wa Samaki,
  • Ufugaji wa samaki,
  • Maadui wa samaki ni,
  • Ubadilishaji wa maji,
  • Ulishaji wa samaki,
  • Mtaji,
  • Fursa zinazoweza jitokeza kwenye maji yanayofugia samaki,

ENEO
Katika ujenzi wa bwawa la samaki  nikipengele ambacho kinatakiwa kuangalia sana.Ni mara chache wahusika wamekuwa wakizingatia kigezo hichi.Swala la eneo linakuwa limebeba vigezo vingi sana kama :


  • mwinuko wa eneo husika ili kuzingatia swala la uingizaji na utoaji wa maji kwenye bwawa litakapokuwa limejengwa,
  • vyanzo vya maji katika sehemu husika,
  • aina ya udongo katika sehemu husika.
  • ukubwa wa eneo husika,na mazingira yake kwa usalama wa zoezi zima la ufugaji wa samaki,
  • fursa nyingine zinazoweza tumika kwa maji yanayokuwa yakibadilishwa kutoka kwenye bwawa. Fursa hizo ni kama kilimo na shughuli nyingine zenye uhitaji wa maji hayo.
Swala hili ni muhimu sana na tunashauri ni vyema kuwasiliana na wataalamu waliobobea kwenye maswala haya ya ufugaji wa samaki kabla ya kuamua kufanya biashara hii ya ufugaji.Wataalamu hao wanaweza kukupa ushauri mzuri wa jinsi gani uyajenge mabwawa ya samaki kulingana na hali ya eneo lako lilivyo na ukubwa wa eneo husika.

MAJI
Maji ni moja ya kigezo kikubwa sana kwenye biashara ya ufugaji wa samaki.
tulibahatika kukutana na msemo mmoja kutoka kwa wataalamu wengi na wafugaji pia kwamba maji ni kila kitu katika ufugaji wa samaki.

Yaani usipozingatia hapa basi ni ngumu kupata matokeo uliyoyatarajia.

๐ŸฌKwenye swala la maji ni vyema kufahamu yafuatayo:๐Ÿฌ๐Ÿ ๐Ÿ 


  • Ni vyema kushirikisha wataalamu kama unataka kupata matokeo mazuri .Hii ni kutokana na ukweli kwamba ufugaji wa samaki wa maji baridi yaani maji yasiyokuwa ya baharini ni vyema wataalamu waweze kupima na kucheki PH na ubora wa maji husika kama yanafaa kwa zoezi hili.Kigezo hichi kifanyike kabla hujaanza zoezi la ujenzi wa bwawa.
  • Pindi utakapokuwa ushaanza zoezi la ufugaji wa samaki ni vyema kabisa kuwasiliana na wataalamu ili waweze kukupa utaratibu sahihi kwa ajili ya kupima Oxygen kama inatosha kwenye bwawa husika hii inachangia sana katika uhai na maisha ya samaki bwawani.
  • Ni vyema kupata utaratibu wa namna ya kupima jotoridi kwenye maji ya bwawa lako hii inatokana na mazingira yetu ya Tanzania kuwa na vipindi mbali mbali katika mikoa tofauti.Sababu hii ni vyema kuzingatia sababu nayo ni sababu kubwa katika ukuaji wake.
  • Sababu hizi zitakusaidia endapo unaanza ufugaji wa samaki ni wakati gani mwafaka wa kubadili maji na kwa kiasi gani kubadili maji yaliyoko kwenye bwawa lako.

kwa utafiti wetu tumeona ni vyema kuhusisha wataalamu ili wakupe mbinu sahihi kwa ajili ufugaji bora wa samaki kibiashara utakaoambatana na matokeo bora.

AINA ZA MABWAWA



Tumegundua zipo aina nyingi za mabwawa ila kwa lugha rahisi tutakupa ufafanuzi mdogo ambao ni:


  • Yapo mabwawa ya kuchimbwa chini na kama ardhi haitwamishi maji basi linachimbwa tu baadae zinafata taratibu nyingine za zoezi la kuandaa uwekaji wa samaki.
  • Yapo mabwawa ya kuchimbwa na kujengewa yamkini kuta zake au kujengewa bwawa zima.
  • Yapo mabwawa mengine ambayo yanajengewa kuanzia usawa wa ardhi ambayo mara nyingi huwa duara.
  • tunashauri pia kuwashirikisha wataalamu watakupa mwanga wa namna wa bwawa la kujenga kigezo kikiwa ni eneo ulilonalo,aina ya udongo ulionao,mtaji wakuanzia na vigezo vingine vidogo.


UJENZI WA BWAWA




Ujenzi wa bwawa unatofautiana kulingana na eneo husika,ukubwa wa mradi unaotaka kuuweka,aina ya udongo,maadui wa samaki walioko kwenye eneo husika.

katika kukupa mwanga wa fursa hii tutakupa hatua kadhaa zinazolenga kwenye ujenzi wa bwawa.

Hatua hizo ni:


  • Kina cha bwawa la samaki mara nyingi hutofautiana Kati ya maingilio ya maji na matoleo ya maji ambapo maingilio ya maji huwa na kina kifupi zaidi kulinganisha na matoleo ya maji ambapo matoleo huwa na kina cha mita  moja na nusu (1,5) ila mara nyingi wataalamu wanasema inategemeana na ukubwa wa bwawa la samaki,
  • Mabwawa mengi kuta zake hujengwa kwenye mwinuko wa wa nyuzi 45 hii inasaidia kurahisisha uvunaji,kuzuia mmomonyoko wa kuta  kwenye bwawa,
  • Kama bwana ni la kuchimba basi ujenzi hufanyika kulingana na maelekezo ya wataalamu ili kuzingatia aina ya udongo iyoko sehemu husika.Ingawa ni vyema kufahamu kama ardhi inapitisha maji basi unaweza tumia polythene sheet ili kuzuia maji yasipotee pia kama ni kujenga basi ni vyema kufahamu kwamba utumiaji wa matofali

Tunashauri ujenzi huu wa bwawa ni vyema kushirikisha wataalamu ili kupata matokeo mazuri kibiashara.

MIFUMO YA UFUGAJI WA SAMAKI ni
Katika ufugaji wa Samaki kwenye mabwawa mifumo ya ufugaji wa Samaki mayo imegawanyika katika sehemu kuu Tatu;

Mfumo wa extensive: 

๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ
Mfumo huu unahusisha utumiaji wa vitu asili Kama chakula kinachopatikana  ndani ya maji,uangalizi wake ni mdogo,pia uwezekano wa Samaki kushambuliwa na magonjwa pia ni mdogo,uwekezaji wake ni mdogo na uvunaji wake pia ni mdogo

Mfumo wa semi intensive:

๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ 
 Mfumo huu unahusisha teknolojia ya Kati ambayo chakula cha asili ndani ya maji na urutubishaji wa bwawa una husika kwa kiasi fulani,pia chakula za ziada kina ongezwa, uhudumiaji wake kwa ujumla ni wa saizi ya kati kama uangalizi, udhibiti wa magonjwa , uwekezaji wake na pia uvunaji wake ni wa wastani

Mfumo wa intensive: huu

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ
 unahusisha utumiaji wa teknolojia ya hali ya juu Sana ambayo urutubishaji wa bwawa unatumika, pia chakula kinachotumika ni kile kilicho fanyiwa kanuni za kisayansi ili kupata uwiano halisi wa virutubisho vyote vinavyohitajika kwa ukuaji wa samaki,uhudumiaji wake ni wa hali ya juu Kama kuangalia ubora wa maji kila wakati,huduma zote hufanyika kwa ustadi wa hali ya juu sana Kama kudhibiti magonjwa,pia uwekezaji na mavuno yake ni ya hali ya juu sana

UFUGAJI WA SAMAKI


๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿ Kipengele hiki ni miongoni mwa vipengele mama katika ufugaji wa samaki kwani kitakuongoza kujua uamue ufuge aina gani ya ufugaji ili kuweza kujipatia kipato,kujipatia kitoweo na kukidhi matakwa ya mahitaji ya samaki kwa wateja wako .Ufugaji Upo wa aina mbili:

Monoculture: 

๐Ÿฌ
UFUGAJI unahusisha aina moja ya samaki kukaa katika bwawa pia waweza kufanyika katika maji baridi au maji ya chumvi.Tukichukulua mfano wa maji baridi waweza kufuga sato(tilapia species) tuu katika bwawa au kambale(clarius species)

Polyculture:

๐Ÿฌ๐Ÿ 
 aina hii ya ufugaji unahusisha kuchanganya aina mbili au zaidi kwenye bwawa moja .tukichukulia mfano wa maji baridi waweza kufuga samaki aina ya sato(tilapia)  na samaki aina ya kambale(clarius) kwenye bwawa.

MAADUI WA SAMAKI

✍️✍️✍️๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡Katika ufugaji wa samaki kwenye mabwawa ya samaki changamoto kubwa ni maadui wa samaki.Zipo njia nyingi za kujikinga na changamoto.

Maadui wa samaki kwenye mabwawa ni:

  • ๐Ÿ‘‰Vyura
  • ๐Ÿ‘‰Kenge
  • ๐Ÿ‘‰Nyoka
  • ๐Ÿ‘‰Ndege

Tumegundua baadhi ya maadui wakubwa wa samaki kwenye mabwawa ni hao walio orodheshwa hapo juu.Kujikinga na maadui hao ni vyema yafanyike yafuatayo:

Kujikinga na vyura ni vyema kuhakikisha unaweka uzio wa fensi ya waya kuzunguka bwawa lako kama unauwezo wakufanya hivyo,fensi hii hakikisha iwe ya vitundu vidogo ili kuweza kuwa kizuizi kwa jamii hii.

Jamii ya Kenge pia inaweza kuzuiwa na aina hii ya fensi na ni vyema kuhakikisha huachi uotaji wa kichaka kikubwa karibu na eneo la bwawa ili kuepusha mazalia na maficho ya viumbe hawa.

Kwa kizuizi cha ndege ingawa wengi wanatumia urutubishaji wa maji ya samaki kwa kutumia mbolea ili kusaidia pia katika chakula na kinga ya samaki dhidi ya maadui wake kama ndege,utaratibu wa kufunga kamba zinazokuwa na umbali mdogo unaoachanisha nyuzi na nyuzi.

Hii itatengeneza mazingira magumu kwa jamii zozote za ndege kuingia kwenye bwawa na kunyakua samaki.

Ni vyema kuhakikisha unaweka wavu wa fensi mkubwa na mlango kama eneo lako halina usalama ili kuondoa hatarishi za maisha kwa watoto au binadamu wengine ili wasitumbukie kwenye bwawa.

✍️✍️✍️๐Ÿ ๐Ÿ ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ

UBADILISHAJI WA MAJI
Kama wanavyosema maji ni kila kitu kwa samaki, tumegundua pia zoezi la kubadili maji linabidi lizingatiwe sana ili kupata matokeo mazuri. imegundua kuwa vipo vigezo vingi vinavyotakiwa kuangaliwa kama ubora wa maji,joto la maji husika kulingana na eneo na hali ya hewa ya eneo husika,uchafu wa maji kutokana na chakula na alkalinity na acidity ya maji.ni vyema kuvifahamu vitu hivi kitaalamu ili kujua wakati sahihi wa kubadili maji.Suluhisho la zoezi hili ni kushirikisha washauri wa maswala la ufugaji wa samaki na wataalamu wa kitengo hichi.

ULISHAJI WA SAMAKI

✍️✍️✍️✍️✍️๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Wataalamu wengi wana njia (formula)  tofauti tofauti za ulishaji wa samaki lakini vigezo vikubwa vikiwa ni ukubwa wa samaki husika,idadi ya samaki kwenye bwawa husika,asilimia za uwezekano wa samaki kuishi,na kasi ya kula.Kwa mfano fursatz.com baada ya kumtembele mfugaji mmoja anayefuga idadi ya samaki 670 njia yake ya ulishaji kwa samaki wadogo waliokuwa wana uzito wa gram 2 (2g) ulikuwa:

=670*(96/100)*2g*(8/100)

=102.912g ambao wastani inakuwa ni 100g

Ni vyema kuhakikisha samaki wanapewa kiasi wanachomaliza kipengele cha uzito kikizingatiwa,hii itasaidia kupunguza chakula kubaki kwenye bwawa na kusababisha uchafuzi mkubwa wa maji na ikichangia kupoteza gharama kubwa za ulishaji.

Watu wengi wanapenda kuulinganisha gharama za ulishaji ni vyema kufata utaratibu unaoshauriwa na wataalamu husika kigezo cha kiasi kinachotakiwa na samaki wapewe.Kwa mfano katika gram 100 zilizopatikana hapo juu kwa samaki wa wiki 2 inabidi kigawanywe mara nne katika uwiano wa saambili,nne,sita na kumi jioni.

Wataalamu wanashauri kuwa ni vyema kutowapa chakula wakati wa mvua,wakati wa usiku  na wakati wa wingu zito hii itasaidia kuto kupoteza chakula bure na kupunguza gharama kwa sababu wakati huu samaki ulaji wao ni mdogo sana.

 MTAJI๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿคซ๐Ÿคซ๐Ÿ—ฃ️๐Ÿ—ฃ️



Kipengele hichi ndicho kinawapa changamoto wapenda fursa. inashauri ni bora kujitadhimini mtaji wa kiasi gani unao na una lengo la kuzalisha kiasi gani na kufahamu gharama za uendeshaji.Maswala ya kuwashirikisha wataalamu itakusaidi kufahamu ni gharama gani zitakazo kwenda kwenye:


  • Mpangilio wa eneo,
  • Upimaji wa maji,
  • Uchimbaji wa visima kama kunaulazma,
  • Upatikanaji wa maji kama ni kutoa kutoka kwenye vyanzo vya maji,
  • Uchimbaji wa bwawa,
  • Ujenzi wa bwawa kama kuna ulazma,
  • Ujenzi wa vizuizi vya maadui wa samaki ili kuhakikisha usalama wa samaki mwenyewe na uwekezaji wa mwekezaji,
  • Gharama ya vifaranga kulingana na ukubwa wa bwawa,
  • Gharama za chakula cha samaki
  • Gharama za uendeshaji wa mradi wa samaki n.k
  • Kama mwekezaji ni vyema kufahamu vitu hivi ili kuweza kujua kwa makadirio gharama za uwekezaji ni kiasi gani na nini mategemeo yako kwenye uwekezaji wako.


FURSA ZINAZOWEZA JITOKEZA KWENYE MAJI YANAYOFUGIA SAMAKI
Katika kila fursa mara nyingi ukiangalia kwa makini kuna fursa nyingine.Nijukumu la kila mtu kuangalia kwa makini kila fursa changamoto inayojitokeza yamkini ni mwanzo wa fursa nyingine.

Maji yanayokuwa yanatolewa kwenye bwawa la samaki yanakuwa na virutubisho vingi katika umwagiliaji wa mazao mbali mbali.

Ni vyema kufahamu kwa kupima udongo wa eneo lako ili kufahamu mazao gani yanastawi vyema hii itakupa fursa ya kufanya kilimo kingine cha umwagiliaji kwa kutumia maji yanayobadilishwa toka kwenye bwawa lako.Fursa 

hiyo inaweza kuwa ya kilimo cha:

  • Mapapi,
  • Maembe,
  • Migomba ya ndizi,
  • Nyanya,
  • Vitunguu,
  • Pilipili hoho,
  • Mboga mboga za majani n.k

Ni vyema kufanya upimaji wa udongo toka sehemu husika ili kujua fursa itakayo ambatana na ufugaji wa samaki nah ii itasaidia kuweka maji yako safi kwa kigezo kwamba kama zoezi la umwagiliaji litakuwa ni la mara kwa mara basi maji yatakuwa yanatumika ya bwawani kupitia outlet uliyoijenga na kutumia inlet utakuwa unaongeza maji masafi.

Hii itasaidia kuweka na kudumisha maji yako yawe masafi zaidi

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰SOMA mbinu za kufanikiwa Kwenye ujasiriamali

๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐Ÿฌ UFUGAJI AJIRA YANGU๐ŸŸ๐ŸŸ

Sunday, April 26, 2020

KANUNI ZA KUFANIKIWA KWENYE UJASIRIAMALI๐ŸŽฏ



๐ŸŒWengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo.

๐ŸŽฏIkiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali.

1. Kuwa mtatuzi wa matatizo

✍️✍️Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”

2. Kuwa na maono

✍️✍️Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐ŸŒฑ“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”๐ŸŒฑ

3. Chagua washirika au timu sahihi na wenye fikra chanya.


✍️✍️Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡


4. Toa huduma au bidhaa yenye tija

✍️✍️Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

5. Fahamu na jali wateja wanatakani .

✍️✍️✍️Ikiwa wewe ni mjasiriamali, basi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji wewe. Fahamu kuwa wewe kama mjasiriamali, ndiye unaye wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha mambo haya kuhusu wateja:

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏFahamu wanataka nini.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏSikiliza maoni na ushauri wao.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏHakikisha unakamilisha mahitaji yao.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏTumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏMfanye mteja aone unamthamini.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏMfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla ya pesa.

Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

6. ๐Ÿ’ฐTumia pesa vyema๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ

✍️✍️Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.


Ni wazi kuwa matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Unaweza pia kujifunza wewe mwenyewe jinsi ya kutunza na kutumia pesa vyema; unaweza pia kutumia programu za bure za kompyuta kama vile Wave app kutunza mahesabu yako.

7. Jifunze kusema hapana

✍️✍️“Hapana” ni jibu dogo lakini lenye manufaa makubwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kusema hapana kwani itakutenga na mambo au mipango isiyokuwa na ulazima.

Kuna watu, mipango, vitu au hata tabia ambazo zinaweza kukuathiri vibaya sana kwenye ujasiriamali wako. Hivyo kusema hapana kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na mambo haya.


8.Tumia teknolojia kukuza huduma yako.


✍️✍️Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia, hivyo wewe kama mjasiriamali huwezi kujitenga nao. Kwa kupitia teknolojia kama vile simu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza mauzo ya huduma au bidhaa zako.

Hakikisha wewe kama mjasiriamali unakuwa karibu na wateja wako ili kutatua shida na mahitaji yao; pia hakikisha unajifunza mbinu bora za kufanya biashara kupitia mtandao.


9. Fahamu soko๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

✍️✍️✍️Kanuni mojawapo ya kuongeza mauzo yako kama mjasiriamali ni kulifahamu soko vyema. Hakikisha huduma au bidhaa unayoitoa inakidhi mahitaji na inafika kwenye soko stahiki.

Kwa mfano ikiwa wewe ni mzalishaji wa mayai, lakini eneo ulilopo soko ni duni, basi tafuta eneo jingine ambalo soko la bidhaa hii ni nzuri. Ikiwa wewe huwezi kwenda, unaweza kutafuta mtu kwenye eneo lenye soko zuri akakuuzia bidhaa yako na ukampa gawio fulani.

Kwa kufanya hivi utaweza kulenga soko na kujiongezea faida zaidi wewe kama mjasiriamali.

10. Ongeza maarifa

✍️✍️Kwanza nikupongeze kwa kusoma makala hii, ni wajasiriamali wachache sana ndiyo hupenda kusoma makala na vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa. Ni muhimu sana kila mara ukajizoesha kujiongezea maarifa, hasa ya ujasiriamali pamoja na kile unachokifanya; hili liitakuwezesha kuwa na tija na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Unaweza kusoma vitabu, majarida na tovuti mbalimbali (kama fahamuhili.com) ili kuongeza maarifa yako.

11. Jifunze kutokana na makosa

✍️✍️Moja ya kanuni inayozingatiwa na wajasiriamali waliofanikiwa ni kujifunza kutokana na makosa. Makosa ni shule nzuri sana kwa kila mtu hasa wajasiriamali. Ikiwa uliwekeza ukapata hasara, basi jifunze nini hasa kilikuwa chanzo cha hasara ili mbeleni uweze kukiepuka. Usikubali kukwamishwa na makosa, bali yawe ni hamasa kwako ya kuendelea mbele zaidi.

“Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo”
Bill Ackman

12. Jifunze kwa waliofanikiwa

✍️✍️Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa sababu wanajifunza kwa walioshindwa. Walioshindwa wana maneno mengi, hasa ya kukatisha tamaa kama vile hili haliwezekani, hili linahitaji pesa nyingi sana, mimi lilinishinda, linachosha, lina faida ndogo, kuna wengi wanaolifanya, fulani alishindwa n.k.

Wewe kama mjasiriamali, epuka watu hawa na ujifunze kwa waliofanikiwa, fahamu walitatua vipi changamoto walizokabiliana nazo pamoja na mipango waliyoitumia hadi wakafika hapo walipo.

13. Tumia muda vizuri

✍️✍️✍️Hakuna mtu mwenye zaidi ya saa 24 duniani; lakini mwingine muda unamtosha wakati mwingine analalamika  muda haumtoshi. Ni wazi kuwa mpangilio au matumizi mabaya ya muda ndiyo husababisha changamoto hii. Wewe kama mjasiriamali ni muhimu ukaondoa mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye ratiba yako. Tambua ni kitu gani ni cha muhimu zaidi na ukifanye kwa wakati.


14. Weka vipaumbele

✍️✍️Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kujiwekea vipaumbele; vipaumbele vitakuwezesha kubaini ni kipi kianze na ni kipi kifuate kutokana na umuhimu wake.

Kwa mfano ikiwa kuna wateja walipata shida kupata huduma au bidhaa yako, maliza kwanza swala hili kabla ya kuendelea kuweka jitihada za kuuza bidhaa mpya. Kwa kufanya hivi utaweza kufanya mambo kutokana na umuhimu wake, jambo ambalo litakuwezesha kukua.

15. Usikate tamaa๐ŸŽฏ๐ŸŽฏ

๐Ÿ’ช๐Ÿ’ชNi wazi kuwa katika safari ya ujasiriamali utakutana na changamoto mbalimbali. Jambo la msingi ni kukumbuka kanuni hii kuwa usikate tamaa. Tumia changamoto kama chachu ya kukuhamasisha kufanya bidii zaidi na usirudi nyuma.

Changamoto zipo leo na kesho lakini keshokutwa hazitakuwepo tena; jambo unalotakiwa kufanya ni kutazama lengo lako na kufanya bidii kila kukikucha kuzikabili changamoto husika ili ufikie lengo lako.

“Siri ya mafanikio yetu ni kutokukata tamaa

๐ŸŽฏUNAWEZA KUWA UNACHOTAKA๐ŸŽฏ

Saturday, April 25, 2020

๐ŸŒฑKILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI ,ONGEZA KIPATO HARAKA

๐ŸŒฑVitunguu ni mojawapo ya zo muhimu ambalo hulimwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi Tanzania. Zao la vitunguu hulimwa kama zao la bishara katika maeneo mbalimbali nchini na huwapatia watu kipato kikubwa ambacho huwasadia katika kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi na kusaidia katika kupambana na umasikini.

Vitunguu hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza harufu nzuri na ladha katika vyakula.  Hutumika katika utengenezaji wa supu, siki ,kachumbari nk. Majani ya vitunguu yana madini ya chokaa na wanga kwa wingi. Vilevile virutubisho vingine kama protini, chuma na ascorbic acidi hupatikana katika vitunguu.

๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟNchini mwetu vitunguu hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tanga,  Arusha sehemu za Mang’ora na Babati, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha , Mara , Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo ,Mbeya Kilimanjaro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Singida.

Katika shamba lililo hudumiwa vizuri na kupandwa katika hali ya hewa na aina ya mbengu. Vitunguu hutoa kiasi cha tani (10) hadi 16 kwa ekari moja.

๐ŸŒ๐ŸŒ๐ŸŒMazingira๐ŸŒ๐ŸŒ๐ŸŒ

Vitunguu husitawi vizuri katika maeneo yenye miinuko kuanzia mita 800 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari. Hupendelea hali ya ubaridi kiasi hususani wakati wa kuotesha mbegu kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa kwa miche iliyoko kwenye kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 27°C. Joto la juu hufanikisha utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji. Hivyo ni vema vitunguu vioteshwe wakati wa baridi ili viweze kuvunwa wakati wa Joto.

✍️✍️Udongo: ๐ŸŒฑ๐ŸŒฑ
Huhitaji udongo tifutifu wenye rutuba nyingi usiotuamisha maji na usiopasukapasuka. Huhitai udongo ulio katika kipimo cha pH kati ya 6.0 na 7.0

Aina za vitunguu vinavyoshauriwa kuoteshwa katika ukanda wa Joto ni Red Creole, Texas Grano, Tropical Red F1 hybrid, Singida local na Pretoria Grano.


✍️✍️Upandaji na Uoteshaji miche๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mbegu za vitunguu huoteshwa kwanza kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri takribani wiki mbili. Vitunguu maji huoteshwa zaidi kwa kutumia mbegu kwenye kitalu na kisha kupandikizwa shambani.

Kabla ya kuzipanda mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita moja (sentimeta 100) na urefu wowote kutokana na mahitaji yako.  Weka mbolea aina ya samadi kiasi cha ndoo moja ukiichanganya vizuri na udongo kwa kila mita ya mraba moja.

Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa miche ya kutosha kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba. Mwagilia kitalu kwa maji ya kutosha siku moja kabla ya kupanda mbegu.

Panda mbegu katika misitari yenye nafasi ya sentimita10 hadi 15 kutoka msitari hadi msitari Na kina cha sentimita moja kwa kumiminwa polepole kwenye mistari/mifereji iliyoandaliwa vizuri. Kisha fukia kwa kunyunyuzia udongo juu ya mbegu zilizoko kwenye mifereji.

Weka matandazo kisha mwagilia mara mbili kila siku(asubuhi na Jioni) hadi mbegu zitakapoota.Mbegu bora  huota baada ya siku 7 hadi 12 kutegema hali ya hewa. Mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka siku 21 udongo unapokuwa wa baridi sana na hali ya hewa ikiwa nzuri, mbegu huota mapema zaidi, hata ndani ya siku 4.

✍️✍️Kuandaa shamba๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Tayarisha shamba vizuri mwezi mmoja kabla ya kupandikiza. Udongo utifuliwe vizuri kwenye urefu kina cha sentimita 30 na ulainishwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. Mbolea za asili ziwekwe shambani ili kuufanya udongo ushikamane vizuri na uweze kuhifadhi mbegu. .Kisha tengeneza matuta au majaruba kufuatana na nafasi za kupandia ili kurahisisha umwagiliaji.

✍️✍️Kupandikiza vitunguu shambani๐Ÿ‘‡


Miche huwa tayari kupandikizwa shambani wiki 6 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche iliyo tayari huwa na urefu wa sentimita 12 hadi 15 na unene 1/2 au 3/4 ya kalamu ya risasi kwenye shina.

Kabla ya kupandikiza loanisha kitalu ili kuepuka kukata mizizi. Ng’oa miche kwa kutumia kijiti au chombo kingne na punguza majani na mizizi ili kusaidia kuzuia upotevu wa maji. Wakati wa upandikizaji chagua miche iliyo na afya nzuri ambayo haikushambuliwa na magonjwa na wadudu. Miche ipandwe wakati wa asubuhi na jioni ili kuepuka jua na joto kali linaloweza kuidhoofisha miche. Miche ipandikizwe kwenye nafasi ya upana wa sentimita 20 hadi 30 na nafasi ndani ya mstari ni sentimita 10 hadi 15. Baada ya kupandikiza mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka miche itakapo shika vizuri.

✍️✍️UTUNZAJI WA SHAMBA๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

A). Mbolea

Vitunguu vina hitaji udongo wenye rutuba ya kutosha ili viweze kusitawi vizuri.mbolea za kukuzia kama vile CAN au S/A ziwekwe shambani wiki 3 na ya 6 baada ya kupandikiza. Kiasi cha mifuko 3 au 4 kinatosha kuwekwa kwenye shamba la ukubwa wa hecta moja. Mbolea iwekwe katika kiwango sahihi yaani kifuniko kimoja cha soda (gram 5) kwa mche. Mbolea iwekwe kwenye mistari bila kugusa mche.

 

Upungufu wa kirutubisho cha Nitrojeni unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa kitunguu. Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa kitunguu na unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora.

B). Umwagiliaji:

Ili kupata mavuno bora shamba linatakiwa kuwa na maji ya kutosha kila wakati. Umwagiliaji wa maji yanayokwenda chini kiasi cha sentimeta moja (1cm) au zaidi kwa wiki ni mzuri kwa kupata vitunguu vikubwa. Epuka umwagiliaji kupita kiasi au pungufu kwani hali hii huweza kusababisha mipasuko. Punguza kumwagilia wakati vitunguu vinapokomaa kwani husababisha vitunguu vinavyokomaa kuoza.

C). PALIZI (UTHIBITI WA MAGUGU)

Magugu yaondolewe mara kwa mara kila yanapojitokeza hasa miche inapokuwa michanga.  Ukuaji na mavuno yanaathirika sana endapo magugu hayatadhibitiwa mapema. Magugu yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe dogo la mkono. Wakati mwingine ni mchanganyiko wa madawa, jembe la mkono na kungolea kwa mkono.

MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

A). MAGONJWA

i.        Ubwiri vinyoya juu(powdery mildew) na wa chini (Downy mildew)

Huu husababishwa na ukungu na hupendelea hali ya unyevu nyevu. Hushambulia  hushambulia majani ya mimea iliyo shamabani na hata miche michanga. Dalili zake Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati za baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na huweza kupeperushwa mbali na upepo.

Nyunyuzia dawa mojawapo zifuatazo kuzuia ukungu: - Dithane-M45, Ridomil, Topsin M70 na Cupric Hydroxide (Champion).

Ugonjwa wa doa la pinki (Purple blotch)

Huu nao ni ugonjwa uletwao na Ukungu na hushambulia majani, shingo na vitunguu vilivyokomaa. Huanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha linaongezeka ukubwa na kufanya baka la rangi ya Zambarau ambalo huonekana katikati ya jani ambalo baadaye huwa jeusi. Shina lililoshambuliwa hulegea na kuanguka katika wiki ya tatu au ya nne baada ya dalili za ugonjwa kuonekana. Vitunguu vilivyokomaa huoza kuanzia shingoni na hugeuka rangi kuwa ya njano iliyochanganyika na nyekundu.

Zuia ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:-

 Kupanda aina ya vitunguu visivyoshambuliwazidi na ugonjwa huu (Red Creole) Kubadilisha mazaoVuna vitunguu kwa wakati sahihiMatumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine,matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu uongeza mlipuko wa magonjwa.Viatilifu kama vile MancozebDithane-M45, Ridomil, Topsin M70 na Cupric Hydroxide (Champion).

i.        Kuoza kwa shingo (Neckrot)

Husababishwa na ukungu na hupendelea vile vile hali ya unyevunyevu. Hushambulia zaidi vitunguu vilivyohifadhiwa. Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa laini, hubonyea na huonekana kama vilivyopikwa. Huanzia kwenye shingo na baadaye huenea kwenye kitunguu chote na kufunikwa na ukungu wa kijivu.

Namna ya kuzuia:-

Vuna vitunguu kwa wakati sahihi Kubadilisha mazao   Tumia njia sahihi wakati wa kuvuna, epuka kuchubua au kukikwaruza wakati wa kuvuna  Kausha vitunguu vizuri baada ya kuvuna  Hifadhi vitunguu sehemu zisizo na unyevu mwingi

. UDHIBITI WA WADUDU

Sata (Cutworms) Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu (Onion maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms), Bungua weupe (White grub),ni miongoni mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.

Tumia dawa zilizothibitishwa na wataalamu.

๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€Uvunaji๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Vitunguu huwa tayari kuvunwa baada ya miezi mitatu mpaka mitano (siku 90 mpaka 150) tangu kusia mbegu kutegemeana na aina na hali ya hewa ya eneo husika. Kabla ya kuvuna mkulima anaweza kuanza maandalizi ya kuvuna mwezi mmoja kabla kwa kuondoa udongo polepole kwenye kitunguu ili kusidia ukaushaji mzuri. Vitunguu vianze kuvunwa pale ambapo asilimia 50 hadi 75 ya vitunguu huonesha kulegea au kunyauka. Vitunguu huvunwa kwa hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa.

๐Ÿ—ž️๐Ÿ—ž️  KUHIFADHI๐Ÿ“ฅ๐Ÿ“ฅ

Vitunguu vilivyovunwa vikaushwe vizuri kabla ya kuvihifadhi. Vihifadhiwe katika eneo lenye hewa ya kutosha, isiyokuwa na unyevu wala jua kali. Vitutnguu vihifadhiwe kwa kuvitandaza juu ya chanja au kwa kufunga mashina yake yaliyokauka vizuri kwa kuyaning’iniza sehemu ya kuhifadhia. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au zaidi bila kuharibika.

๐Ÿ“’๐Ÿ“’๐Ÿ“’Mavuno๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ


Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja nav hali ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya tani 30 hadi 40 kwa hekta moja.
✍️✍️Tukutane sokoni๐ŸŽ
✍️✍️kilimo ajira yangu๐Ÿ’“๐Ÿ’“