Sunday, April 26, 2020

KANUNI ZA KUFANIKIWA KWENYE UJASIRIAMALI🎯



🌍Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo.

🎯Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali.

1. Kuwa mtatuzi wa matatizo

✍️✍️Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.👇👇

“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”

2. Kuwa na maono

✍️✍️Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.👇👇

🌱“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”🌱

3. Chagua washirika au timu sahihi na wenye fikra chanya.


✍️✍️Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.👇👇


4. Toa huduma au bidhaa yenye tija

✍️✍️Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.👇👇

5. Fahamu na jali wateja wanatakani .

✍️✍️✍️Ikiwa wewe ni mjasiriamali, basi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji wewe. Fahamu kuwa wewe kama mjasiriamali, ndiye unaye wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha mambo haya kuhusu wateja:

🎯🎯Fahamu wanataka nini.

🎯🎯Sikiliza maoni na ushauri wao.

🎯🎯Hakikisha unakamilisha mahitaji yao.

🎯🎯Tumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.

🎯🎯Mfanye mteja aone unamthamini.

🎯🎯Mfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla ya pesa.

Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.👇👇

6. 💰Tumia pesa vyema💰💰

✍️✍️Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.


Ni wazi kuwa matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Unaweza pia kujifunza wewe mwenyewe jinsi ya kutunza na kutumia pesa vyema; unaweza pia kutumia programu za bure za kompyuta kama vile Wave app kutunza mahesabu yako.

7. Jifunze kusema hapana

✍️✍️“Hapana” ni jibu dogo lakini lenye manufaa makubwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kusema hapana kwani itakutenga na mambo au mipango isiyokuwa na ulazima.

Kuna watu, mipango, vitu au hata tabia ambazo zinaweza kukuathiri vibaya sana kwenye ujasiriamali wako. Hivyo kusema hapana kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na mambo haya.


8.Tumia teknolojia kukuza huduma yako.


✍️✍️Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia, hivyo wewe kama mjasiriamali huwezi kujitenga nao. Kwa kupitia teknolojia kama vile simu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza mauzo ya huduma au bidhaa zako.

Hakikisha wewe kama mjasiriamali unakuwa karibu na wateja wako ili kutatua shida na mahitaji yao; pia hakikisha unajifunza mbinu bora za kufanya biashara kupitia mtandao.


9. Fahamu soko🇹🇿🇹🇿

✍️✍️✍️Kanuni mojawapo ya kuongeza mauzo yako kama mjasiriamali ni kulifahamu soko vyema. Hakikisha huduma au bidhaa unayoitoa inakidhi mahitaji na inafika kwenye soko stahiki.

Kwa mfano ikiwa wewe ni mzalishaji wa mayai, lakini eneo ulilopo soko ni duni, basi tafuta eneo jingine ambalo soko la bidhaa hii ni nzuri. Ikiwa wewe huwezi kwenda, unaweza kutafuta mtu kwenye eneo lenye soko zuri akakuuzia bidhaa yako na ukampa gawio fulani.

Kwa kufanya hivi utaweza kulenga soko na kujiongezea faida zaidi wewe kama mjasiriamali.

10. Ongeza maarifa

✍️✍️Kwanza nikupongeze kwa kusoma makala hii, ni wajasiriamali wachache sana ndiyo hupenda kusoma makala na vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa. Ni muhimu sana kila mara ukajizoesha kujiongezea maarifa, hasa ya ujasiriamali pamoja na kile unachokifanya; hili liitakuwezesha kuwa na tija na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Unaweza kusoma vitabu, majarida na tovuti mbalimbali (kama fahamuhili.com) ili kuongeza maarifa yako.

11. Jifunze kutokana na makosa

✍️✍️Moja ya kanuni inayozingatiwa na wajasiriamali waliofanikiwa ni kujifunza kutokana na makosa. Makosa ni shule nzuri sana kwa kila mtu hasa wajasiriamali. Ikiwa uliwekeza ukapata hasara, basi jifunze nini hasa kilikuwa chanzo cha hasara ili mbeleni uweze kukiepuka. Usikubali kukwamishwa na makosa, bali yawe ni hamasa kwako ya kuendelea mbele zaidi.

“Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo”
Bill Ackman

12. Jifunze kwa waliofanikiwa

✍️✍️Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa sababu wanajifunza kwa walioshindwa. Walioshindwa wana maneno mengi, hasa ya kukatisha tamaa kama vile hili haliwezekani, hili linahitaji pesa nyingi sana, mimi lilinishinda, linachosha, lina faida ndogo, kuna wengi wanaolifanya, fulani alishindwa n.k.

Wewe kama mjasiriamali, epuka watu hawa na ujifunze kwa waliofanikiwa, fahamu walitatua vipi changamoto walizokabiliana nazo pamoja na mipango waliyoitumia hadi wakafika hapo walipo.

13. Tumia muda vizuri

✍️✍️✍️Hakuna mtu mwenye zaidi ya saa 24 duniani; lakini mwingine muda unamtosha wakati mwingine analalamika  muda haumtoshi. Ni wazi kuwa mpangilio au matumizi mabaya ya muda ndiyo husababisha changamoto hii. Wewe kama mjasiriamali ni muhimu ukaondoa mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye ratiba yako. Tambua ni kitu gani ni cha muhimu zaidi na ukifanye kwa wakati.


14. Weka vipaumbele

✍️✍️Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kujiwekea vipaumbele; vipaumbele vitakuwezesha kubaini ni kipi kianze na ni kipi kifuate kutokana na umuhimu wake.

Kwa mfano ikiwa kuna wateja walipata shida kupata huduma au bidhaa yako, maliza kwanza swala hili kabla ya kuendelea kuweka jitihada za kuuza bidhaa mpya. Kwa kufanya hivi utaweza kufanya mambo kutokana na umuhimu wake, jambo ambalo litakuwezesha kukua.

15. Usikate tamaa🎯🎯

💪💪Ni wazi kuwa katika safari ya ujasiriamali utakutana na changamoto mbalimbali. Jambo la msingi ni kukumbuka kanuni hii kuwa usikate tamaa. Tumia changamoto kama chachu ya kukuhamasisha kufanya bidii zaidi na usirudi nyuma.

Changamoto zipo leo na kesho lakini keshokutwa hazitakuwepo tena; jambo unalotakiwa kufanya ni kutazama lengo lako na kufanya bidii kila kukikucha kuzikabili changamoto husika ili ufikie lengo lako.

“Siri ya mafanikio yetu ni kutokukata tamaa

🎯UNAWEZA KUWA UNACHOTAKA🎯

Saturday, April 25, 2020

🌱KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI ,ONGEZA KIPATO HARAKA

🌱Vitunguu ni mojawapo ya zo muhimu ambalo hulimwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi Tanzania. Zao la vitunguu hulimwa kama zao la bishara katika maeneo mbalimbali nchini na huwapatia watu kipato kikubwa ambacho huwasadia katika kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi na kusaidia katika kupambana na umasikini.

Vitunguu hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza harufu nzuri na ladha katika vyakula.  Hutumika katika utengenezaji wa supu, siki ,kachumbari nk. Majani ya vitunguu yana madini ya chokaa na wanga kwa wingi. Vilevile virutubisho vingine kama protini, chuma na ascorbic acidi hupatikana katika vitunguu.

🇹🇿🇹🇿Nchini mwetu vitunguu hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tanga,  Arusha sehemu za Mang’ora na Babati, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha , Mara , Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo ,Mbeya Kilimanjaro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Singida.

Katika shamba lililo hudumiwa vizuri na kupandwa katika hali ya hewa na aina ya mbengu. Vitunguu hutoa kiasi cha tani (10) hadi 16 kwa ekari moja.

🌏🌏🌏Mazingira🌏🌏🌏

Vitunguu husitawi vizuri katika maeneo yenye miinuko kuanzia mita 800 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari. Hupendelea hali ya ubaridi kiasi hususani wakati wa kuotesha mbegu kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa kwa miche iliyoko kwenye kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 27°C. Joto la juu hufanikisha utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji. Hivyo ni vema vitunguu vioteshwe wakati wa baridi ili viweze kuvunwa wakati wa Joto.

✍️✍️Udongo: 🌱🌱
Huhitaji udongo tifutifu wenye rutuba nyingi usiotuamisha maji na usiopasukapasuka. Huhitai udongo ulio katika kipimo cha pH kati ya 6.0 na 7.0

Aina za vitunguu vinavyoshauriwa kuoteshwa katika ukanda wa Joto ni Red Creole, Texas Grano, Tropical Red F1 hybrid, Singida local na Pretoria Grano.


✍️✍️Upandaji na Uoteshaji miche👇👇

Mbegu za vitunguu huoteshwa kwanza kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri takribani wiki mbili. Vitunguu maji huoteshwa zaidi kwa kutumia mbegu kwenye kitalu na kisha kupandikizwa shambani.

Kabla ya kuzipanda mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita moja (sentimeta 100) na urefu wowote kutokana na mahitaji yako.  Weka mbolea aina ya samadi kiasi cha ndoo moja ukiichanganya vizuri na udongo kwa kila mita ya mraba moja.

Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa miche ya kutosha kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba. Mwagilia kitalu kwa maji ya kutosha siku moja kabla ya kupanda mbegu.

Panda mbegu katika misitari yenye nafasi ya sentimita10 hadi 15 kutoka msitari hadi msitari Na kina cha sentimita moja kwa kumiminwa polepole kwenye mistari/mifereji iliyoandaliwa vizuri. Kisha fukia kwa kunyunyuzia udongo juu ya mbegu zilizoko kwenye mifereji.

Weka matandazo kisha mwagilia mara mbili kila siku(asubuhi na Jioni) hadi mbegu zitakapoota.Mbegu bora  huota baada ya siku 7 hadi 12 kutegema hali ya hewa. Mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka siku 21 udongo unapokuwa wa baridi sana na hali ya hewa ikiwa nzuri, mbegu huota mapema zaidi, hata ndani ya siku 4.

✍️✍️Kuandaa shamba👇👇

Tayarisha shamba vizuri mwezi mmoja kabla ya kupandikiza. Udongo utifuliwe vizuri kwenye urefu kina cha sentimita 30 na ulainishwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. Mbolea za asili ziwekwe shambani ili kuufanya udongo ushikamane vizuri na uweze kuhifadhi mbegu. .Kisha tengeneza matuta au majaruba kufuatana na nafasi za kupandia ili kurahisisha umwagiliaji.

✍️✍️Kupandikiza vitunguu shambani👇


Miche huwa tayari kupandikizwa shambani wiki 6 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche iliyo tayari huwa na urefu wa sentimita 12 hadi 15 na unene 1/2 au 3/4 ya kalamu ya risasi kwenye shina.

Kabla ya kupandikiza loanisha kitalu ili kuepuka kukata mizizi. Ng’oa miche kwa kutumia kijiti au chombo kingne na punguza majani na mizizi ili kusaidia kuzuia upotevu wa maji. Wakati wa upandikizaji chagua miche iliyo na afya nzuri ambayo haikushambuliwa na magonjwa na wadudu. Miche ipandwe wakati wa asubuhi na jioni ili kuepuka jua na joto kali linaloweza kuidhoofisha miche. Miche ipandikizwe kwenye nafasi ya upana wa sentimita 20 hadi 30 na nafasi ndani ya mstari ni sentimita 10 hadi 15. Baada ya kupandikiza mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka miche itakapo shika vizuri.

✍️✍️UTUNZAJI WA SHAMBA👇👇

A). Mbolea

Vitunguu vina hitaji udongo wenye rutuba ya kutosha ili viweze kusitawi vizuri.mbolea za kukuzia kama vile CAN au S/A ziwekwe shambani wiki 3 na ya 6 baada ya kupandikiza. Kiasi cha mifuko 3 au 4 kinatosha kuwekwa kwenye shamba la ukubwa wa hecta moja. Mbolea iwekwe katika kiwango sahihi yaani kifuniko kimoja cha soda (gram 5) kwa mche. Mbolea iwekwe kwenye mistari bila kugusa mche.

 

Upungufu wa kirutubisho cha Nitrojeni unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa kitunguu. Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa kitunguu na unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora.

B). Umwagiliaji:

Ili kupata mavuno bora shamba linatakiwa kuwa na maji ya kutosha kila wakati. Umwagiliaji wa maji yanayokwenda chini kiasi cha sentimeta moja (1cm) au zaidi kwa wiki ni mzuri kwa kupata vitunguu vikubwa. Epuka umwagiliaji kupita kiasi au pungufu kwani hali hii huweza kusababisha mipasuko. Punguza kumwagilia wakati vitunguu vinapokomaa kwani husababisha vitunguu vinavyokomaa kuoza.

C). PALIZI (UTHIBITI WA MAGUGU)

Magugu yaondolewe mara kwa mara kila yanapojitokeza hasa miche inapokuwa michanga.  Ukuaji na mavuno yanaathirika sana endapo magugu hayatadhibitiwa mapema. Magugu yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe dogo la mkono. Wakati mwingine ni mchanganyiko wa madawa, jembe la mkono na kungolea kwa mkono.

MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

A). MAGONJWA

i.        Ubwiri vinyoya juu(powdery mildew) na wa chini (Downy mildew)

Huu husababishwa na ukungu na hupendelea hali ya unyevu nyevu. Hushambulia  hushambulia majani ya mimea iliyo shamabani na hata miche michanga. Dalili zake Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati za baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na huweza kupeperushwa mbali na upepo.

Nyunyuzia dawa mojawapo zifuatazo kuzuia ukungu: - Dithane-M45, Ridomil, Topsin M70 na Cupric Hydroxide (Champion).

Ugonjwa wa doa la pinki (Purple blotch)

Huu nao ni ugonjwa uletwao na Ukungu na hushambulia majani, shingo na vitunguu vilivyokomaa. Huanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha linaongezeka ukubwa na kufanya baka la rangi ya Zambarau ambalo huonekana katikati ya jani ambalo baadaye huwa jeusi. Shina lililoshambuliwa hulegea na kuanguka katika wiki ya tatu au ya nne baada ya dalili za ugonjwa kuonekana. Vitunguu vilivyokomaa huoza kuanzia shingoni na hugeuka rangi kuwa ya njano iliyochanganyika na nyekundu.

Zuia ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:-

 Kupanda aina ya vitunguu visivyoshambuliwazidi na ugonjwa huu (Red Creole) Kubadilisha mazaoVuna vitunguu kwa wakati sahihiMatumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine,matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu uongeza mlipuko wa magonjwa.Viatilifu kama vile MancozebDithane-M45, Ridomil, Topsin M70 na Cupric Hydroxide (Champion).

i.        Kuoza kwa shingo (Neckrot)

Husababishwa na ukungu na hupendelea vile vile hali ya unyevunyevu. Hushambulia zaidi vitunguu vilivyohifadhiwa. Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa laini, hubonyea na huonekana kama vilivyopikwa. Huanzia kwenye shingo na baadaye huenea kwenye kitunguu chote na kufunikwa na ukungu wa kijivu.

Namna ya kuzuia:-

Vuna vitunguu kwa wakati sahihi Kubadilisha mazao   Tumia njia sahihi wakati wa kuvuna, epuka kuchubua au kukikwaruza wakati wa kuvuna  Kausha vitunguu vizuri baada ya kuvuna  Hifadhi vitunguu sehemu zisizo na unyevu mwingi

. UDHIBITI WA WADUDU

Sata (Cutworms) Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu (Onion maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms), Bungua weupe (White grub),ni miongoni mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.

Tumia dawa zilizothibitishwa na wataalamu.

😀😀Uvunaji😀😀

Vitunguu huwa tayari kuvunwa baada ya miezi mitatu mpaka mitano (siku 90 mpaka 150) tangu kusia mbegu kutegemeana na aina na hali ya hewa ya eneo husika. Kabla ya kuvuna mkulima anaweza kuanza maandalizi ya kuvuna mwezi mmoja kabla kwa kuondoa udongo polepole kwenye kitunguu ili kusidia ukaushaji mzuri. Vitunguu vianze kuvunwa pale ambapo asilimia 50 hadi 75 ya vitunguu huonesha kulegea au kunyauka. Vitunguu huvunwa kwa hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa.

🗞️🗞️  KUHIFADHI📥📥

Vitunguu vilivyovunwa vikaushwe vizuri kabla ya kuvihifadhi. Vihifadhiwe katika eneo lenye hewa ya kutosha, isiyokuwa na unyevu wala jua kali. Vitutnguu vihifadhiwe kwa kuvitandaza juu ya chanja au kwa kufunga mashina yake yaliyokauka vizuri kwa kuyaning’iniza sehemu ya kuhifadhia. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au zaidi bila kuharibika.

📒📒📒Mavuno💰💰


Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja nav hali ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya tani 30 hadi 40 kwa hekta moja.
✍️✍️Tukutane sokoni🍎
✍️✍️kilimo ajira yangu💓💓

Friday, April 24, 2020

KILIMO CHA VITUNGUU NA UTHIBITI WA MAGONJWA


Leo nimependa tujifunze kuhusiana na jinsi ya kukielekea kilimo cha Vitunguu maji.

Vitunguu ni moja ya zao la bustani linalopea na kutumiwa kwa wingi sana si hapa nchini tu bali duniani kote. Kitunguuu kinachukuwa nafasi ya pili baada ya nyanya. Kitunguu kinatumika katika kachumbari, kama kiungo kwenye kitoweo kama vile Samaki, nyama namboga za majani n.k.

 Majani ya vitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika kuandalia supu.

Aina Bora za Vitunguu Maji

1. NEPTUNE
Neptune
Hii ni mbegu bora zaidi ya kitunguu maji kwa sasa kwani hutoa mavuno mengi zaidi kuanzia tani 20 kwa hekari.
Kina rangi nzuri ya kupendeza
Huwa hakitoi mapacha katika yai la kitunguu.
Umbo lake ni kubwa na la duara.

2. Red Creole
download%2B%25283%2529
Hii ni mbegu bora pia katika zao la kitunguu.  Hutoa mavuno kuanzia tani 13 hadi 23 kwa ekari.

  • Kukomaa- siku 150
  • Shape- Nusu bapa
  • Rangi ya Ganda- Nyekundu
  • Ndani-Nyekundu kahawia

3. Red Bombay
images
Mavuno yake ni sawa na red Creole ila hutofautiana rangi na maisha rufani.
  •  siku-160
  • Shape -Duara
  • Rangi  ya ganda-Nyekundu angavu
  • Rangi ndani-Nyekundu kahawia
4. Texas Grano
images%2B%25282%2529
  • Kukomaa-165
  • Shape -Duara
  • Rangi ya ganda- Njano (kaki)
  • Rangi ndani -Nyeupe

HALI YA HEWA
Vitunguu hustawi maeneo yasiyo na mvua nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na maeneo yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa kwa vitunguu.

UDONGO
Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha, unaoruhusu mizizi kupenya na unaohifadhi unyevu kama vile udongo wa nusu mfinyanzi nusu tifutifu na wenye kiasi cha tindikali ya 5.5-6.5.

UPANDAJI WA MBEGU ZA VITUNGUU KWENYE KITALU.
Hapa kwetu Tanzania upandaji huanza mwezi March hadi Mei kutegemea na msimu wa kilimo ulivyo. Hivyo kilimo hiki huanza mara baada ya mvua kubwa za masika kumalizika. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vitunguu.
Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema katika kitalu. Mbegu zinaweza kutawanywa au kupandwa kwa mistari katika tuta la kitalu.Tengeneza matuta yenye upana wa mita 1 na urefu wowote kutegemea na mahitaji yako.Weka mbolea ya samadi ndoo moja hadi mbili kwa mraba wa mita moja.

Lima tuta kiasi cha sentimita 10-25.
Dnc7iTNUYAA5BTH
Sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 15 kutoka mstari hadi mstari Katika upandaji wa mstari mbegu hupandwa katika nafasi ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari. Gramu 5 (kijiko cha chai) zinatosha kusia eneo la mraba mita moja.
Tandaza nyasi na mwagilia.

Baada ya kupanda mbegu hufunikwa na udongo mwepesi na baadaye matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli miche michanga. Mbegu za vitunguu huota baada ya siku 7 hadi 10.

KIASI CHA MBEGU.
 Kilo 1.5 za mbegu zinatosha hekari moja ya shamba.

KUOMBEKA/KUPANDIKIZA MICHE BUSTANINI.

➡Upandikizaji wa miche ya vitunguu hufanyika baada ya miche kukua na kufikia unene wa Penseli. Mara nyingi miche hii hukaa kwenye kitalu kwa siku 35 -40 baada ya kupandwa.

Usichelewe kuhamishia miche kwani  miche mikubwa huanza kutoa maua badala ya kitunguu (bulbs). Hivyo mara nyingi miche ya namna hii hubaki na suke la maua tu.
Wakati wa kupandikiza usikate wala kupunguza majani. Miche ipandikizwe sm 30 kati ya mstari na mstari na sm 10 kati ya mche na mche.

Upandaji katika bustani hufanyika kwenye mistari katika matuta au kwenye vijaruba.
Vijaruba hutumika katika maeneo tambarare na yenye ukame ili kuhifadhi unyevu baada ya kumwagilia. Sehemu zenye udongo mzito na wenye maji mengi tumia matuta yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm 15 kutoka usawa wa ardhi.

➡KUMBUKA: Pandikiza miche wakati wa asubuhi au jioni na mwagilia maji ya kutosha kisha hakikisha maji hayatuami.

MBOLEA
Weka mbolea ya kukuzia katika wiki ya nne hadi sita baada ya kupandikiza.
Weka mbolea kwenye mstari na hakikisha isigusane na mimea. Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha wakati wa kuweka mbolea. Tumia UREA, CAN au SA.

UMWAGILIAJI
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) Umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba.

Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyo kua. Pia ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna. Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.

MATUMIZI YA MBOLEA.
Kwanza kabisa naomba niseme kuwa kuna kasumba ya watu wengi kuogopa matumizi ya mbolea za viwandani kwa dhwanna ya kwamba mbolea hizo zinaharibu udongo na ardhi kwa ujumla wake:

Kwa mimi niwatoe hofu juu ya hilo kwani si kweli kwamba matumizi ya mbolea za viwandani yanaharibu udongo bali ukweli ni kuwa matumizi mabaya na yasiyofuata utaratibu ya mbolea za viwandani yanaharibu udongo na ardhi kwa ujumla. Nitaandaa makala maalumu ya kujulisha umma ni jinsi gani matumizi ya mbolea hata zisizo za viwandani yanavyoweza kuharibu udongo na ardhi kwa ujumla wake.

Hapa tutaona juu ya makundi ya mbolea na muda/ kipindi cha matumizi  ya mbolea hizo.

1. MBOLEA KUNDI LA KWANZA.

Mbolea za kupandia.
Hizi huwekwa kabla au mara tu ya kuhamishia miche shambani. Mbolea hizi zina lengo la kusaidia ukuaji mzuri wa mifumo ya mzizi (root systems) itakayosaidia mmea kufyonza virutubisho na maji kutoka ktk udongo.

Mbolea hizi zina madini/ kirutubisho kikuu cha fosforasi (P), na huitwa mbolea za fosfeti (Phosphate Fertilizers), kundi hili lina mbolea kama MOP, TSP, DAP, Minjingu n.k.

2. MBOLEA ZA KUKUZIA
Mbolea hizi huwekwa kipindi cha ukuaji wa mmea (vegetative growth) na hua na lengo la kuupa mmea afya na ukuaji mzuri utakaopelekea kuwa na majani mazuri yatakayotengeneza chakula cha kutosha kwaajili ya mmea.
Kirutubisho kikuu katika kundi la mbolea hizi ni Nitrogen (N). Baadhi ya mbolea zilizopo kwenye kundi hili ni pamoja na UREA, SA, CAN n.k.

Pia kwenye kundi hili zipo mbolea za maji zinazopigwa kwenye majani (foliar fertilizers) hujulikana pia kama booster.

3. MBOLEA ZA KUZALISHA/KUKOMAZIA KITUNGU.
Hizi ni zile zinazowekwa kuusaidia mmea wa kitunguu  kutaga  (kutengeneza kitunguu). Mbolea hizi huwekwa mara tu kitunguu kinapoanza kutaga.

Kirutubisho kikuu ni ktk mbolea hizi Potassium. Ili Kituunguu kiweze kujijenga vizuri na kuwa na ubora kinahitaji mbolea zenye madini/ kirutubisho cha Potassium. Mfano wa mbolea zenye virutubisho hichi ni Multi K, MOP (Muriate of Potash) n.k.

INGIA HAPA KUONA MPANGILIO WA MBOLEA KATIKA ZAO LA KITUNGUU MAJI 

Zingatia kwamba ili mbolea ziweze kufanya kazi ni lazima uweke pindi ambapo kuna unyevu ktk udongo na uzingatie kumwagilia mara baada ya kuweka mbolea.
 EPUKA KUMWAGILIA MAJI MENGI KWANI VIRUTUBISHO HUENDA CHINI ZAIDI KTK UDONGO
Hayo ndio makundi makuu ya mbolea, japokua mbolea hizo hujumuisha pia virutubisho vidogo (micro nutrients) ambavyo vinahitajika kwa udogo kwenye mimea, japokua zina kazi muhimu kwenye mimea.

WADUDU WAHARIBIFU NA UDHIBITI WAKE KTK KILIMO CHA VITUNGUU

IFAHAMIKE: Ktk makala hii nimeainisha baadhi tu ya wadudu wasumbufu na namna/ njia chache za udhibiti wake. Pia nakaribisha mchango na namna nyengine juu ya udhibiti wa wadudu hawa.

UDHIBITI RAHISI WA MAGUGU 
katika shamba la kitunguu magugu hudhibitiwa kwa namna mbalimbali kama vile kung'olea, kwa jembe na kwa viuwa gugu.

Fahamu Dawa za kuuwa magugu vizuri zaidi shambani


USHAURI: Ni rahisi na gharama nyepesi zaidi kudhibiti magugu katika shamba la kitunguu kwa kutumia viuwa gugu kwa mda mchache.
TUMIA WILSTOP kudhibiti uotaji ama ukuaji wa magugu siku zisizo zidi tatu baada ya kupandikiza vitunguu shambani.
Hakikisha unatumia WILSTOP  majani ama magugu hayajaota ama kabla hajafikisha majani zaidi ya mawili.

Thiripi (Thrips):
images%2B%25283%2529
Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe. Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.

UDHIBITI
20181015_145250

Thrips huudhibitiwa kwa urahisi zaidi kwa kunyunyuzia dawa iitwayo Dudumectin au Duduwill.

Kimamba:
images%2B%252821%2529
Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.

KIDHIBITI

Wadudu hawa huthibitiwa kwa kunyunyuzia dawa iitwayo Dudumectin, willcron au Duduwill: zote hizi hufanya vizuri.

➡Sota (Cutworms):
images%2B%25284%2529
 Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao.

UDHIBITI
20181015_145230

Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama; Duduwill ambayo hutumika ndani ya wiki 0-7.
Duduwill hutumika kutibu udongo wenye wadudu kama hawa kwa kupulizia katika kitalu pia shambani huwadhibiti vizuri zaidi mara tu wanapooneka.

➡Utitiri wekundu (Red spider mites):
images%2B%252820%2529

Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.

KUDHIBITI
kupulizia dawa za wadudu Dudumectin huwadhibiti vizuri zaidi.

Vipekecha majani (leaf miner):
images%2B%252810%2529
Hawa ni aina ya inzi wadogo, ambao viwavi wake wanashambulia majani, kwa kupekecha na kutengeneza mitandao wa mitaro kwenye majani. Viwavi wanashambulia majani na kusababisha majani kukauka. Upungufu mkubwa wa mazao hutokea.

KUDHIBITI
kupulizia dawa ya wadudu kama Dudumectin au Duduwill .
kuteketeza masalia ya mazao
kutumia mzunguko wa mazao.

MAGONJWA NA UDHIBITI WAKE
Kitunguu ni zao amabalo haliwezi kustahimili magonjwa kwa hakika kama yalivyo baadhi ya mazao mengine, hivyo ni muhimu mkulima wa kitunguu ayafahamu magonjwa yote, dalili na namna ya udhibiti wake kabla hajaanza mradi wa kilimo cha kitunguu rasmi .

Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa sumbufu zaidi ktk vitunguu katika ukanda wa Afrika ya mashariki na Tanzania .

1.➡Baka zambarau (Puple Blotch).
pb

Ungonjwa huu unasababishwa na fangasi au Kuvu na
ugonjwa huu hujitokeza zaidi kipindi cha ukungu mwingi na unyevunyevu mwingi hasa wakati wa masika.

Zaidi ya 70 % ya mazao yanaweza kupotea kama ugonjwa hautadhibitiwa Haraka.

🔼DALILI
-madoa meupe yaliyodidimia huonekana kwenye majani na mashina ya kitunguu shambani.
-rangi ya zambarau kuwepo katikati ya doa jeupe.
-majani huanguka kuanzia juu

🔼UDHIBITI
20181031_174046


  • Panda mbegu safi na fanya kilimo cha mzunguko wa mazao.
  • Teketeza masalia ya kitunguu kilichokuwa na ugonjwa shambani kabla ya msimu mpya.
  • Pulizia dawa mfano  superwill (ya maji) au wilthane.
  • Pulizia dawa ya wilzeb kabla ugonjwa haujatokea.
  •  Kama kinga.


2.➡Kinyausi (Damping – off).
onion-downy-mildew-1L

Ugonjwa huu unasababishwa na fangasi na huenezwa kupitia udongo, mbegu na masalia ya mazao shambani.
Ugonjwa hujitokeza zaidi kitaluni panapokuwa na unyevunyevu mwingi au kuzidisha kiwango cha umwagiliaji hivyo udongo kuwa maji maji muda mrefu.

🔼DALILI
-mbegu huoza kabla hata ya kuota
-kunyauka kwa kiwango kikubwa cha miche ya kitunguu baada ya kuota

🔼Kudhibiti.
20181015_145603
  • Hakikisha mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya wilzeb au wilthane kabla ya kupanda.
  • Kusia mbegu kwa nafasi za kutosha
  • Kuepukana na kubananisha miche kitaluni
  •  Kuepukanana na kumwagilia maji wakati wa jua kali au wakati kuna ukungu
  • pulizia dawa ya super will inatibu na kukinga mmea dhidi magonjwa ya kuvu.


Virusi njano vya vitunguu (Onion yellow Dwarf virus)
ydv


-Ugonjwa huu unasababishwa na virusi na kuenezwa na wadudu aina ya vidukari (wadudu -mafuta).

🔼DALILI
  • Kujikunjakunja kwa majani kwa kutengeneza vinundu na uwepo wa mistari ya rangi ya manjano kwenye majani.
  • Hatimae mmea mzima kudumaa, kujikunja na kufa
🔼Kudhibiti:
  • tumia mbegu safi na bora iliyothibitishwa.
  • Kuweka shamba katika hali ya usafi muda wote
  • Kuzuia wadudu piga dawa inaitwa willcron profenofos au dudumectin kwa ufanyajikazi mzuri 
Ukungu mweusi
(Onion Black Mold)
images%2B%252811%2529

Kisababishi: Aspergillus niger

Ugonjwa huu maranyingi hutokea endapo joto litakua kali ktk mazingira.

🔼DALILI
  • Utando mweusi katika gamba la kitunguu.
  • Kuoza shingo na kirungu


🔼Kudhibiti:
-Hakikisha mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya  wilthane au super will kukinga na piga wilzeb au super will  kabla ya ugonjwa kutokea kama kinga na tiba pia.

3.➡Onion Botrytis leaf blight 
images%2B%252817%2529
Kisababishi : Botrytis allii

Ugonjwa huu huonekana wakati vitunguu vimehifadhiwa na maambukizi huanzia shambani.

DALILI
  • Kudumaa kwa kitunguu shambani
  • Sehemu zilizoathirika hukauka na kufa.
  • Gamba gumu katika shingo ya kitunguu huonekana
🔼TIBU
Tumia Wilthane kutibu ugonjwa huu.

4.➡Ubwiri unyoya
(Onion Downy Mildew)
images%2B%252819%2529

Kisababishi: Peronospora destructor
🔼DALILI
  • Kutokea kwa Madoa ya duara, rangi afifu ya njano kwenye majani makubwa na huenea  mpaka kwenye majani machanga.
  • katika majani majani makubwa, madoa ya njano hufunikwa na ukungu wa rangi ya kijivu.
  • Majani yaliyoathirika hulegea, kusinyaa na kukauka kuanzia kwenye ncha.
  • Hatimae Shina la mbegu huzungukwa na madonda na kusababisha kichwa cha mbegu kuanguka.
🔼Kudhibiti:
  • Safisha shamba ,Panda mbegu safi na zingatia kanuni za umwagiliaji
  • Tumia wilthane au super will kutibu pia wilzeb na super will hutumika kukinga.
Kutu (rust)
Leek%2BRust%2Bcrop%2B%25281%2529

Kisababishi: Puccinia porri

🔼DALILI
  • Majani yalioathirika huwa na madoa ya rangi ya machungwa
  • Baadaye hugeuka na kuwa meusi
  • Majani yaliyoathirika sana huwa ya njano na hatimaye hufa.
KUDHIBITI
  • Tumia super will au wilthane kutibu na kukinga ugonjwa huu.
MAVUNO NA MAUZO
Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganishwa na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri.
Hivi sasa bei ya chini kabisa ya vitunguu kilo moja ni Tsh 1000/= kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo. Ekari moja huvunwa Tani 13 hadi 23 sawa na kg 13,000 hadi 23,000. 
Kama mkulima ukipata soko la uhakika mkulima unaweza kupata hadi 13.5million  hadi  23 millions kwa msimu mmoja.

Friday, April 17, 2020

🍅🍅 KILIMO CHA NYANYA 🌱🌱

🍅🍅Kilimo Bora cha Nyanya; Maandalizi Ya Mbegu, Shamba Na Upandaji Wa Miche
🍅🍅🍅🍅🍅🍅🍅🍅🍅

✍️✍️ Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote:

Utangulizi:
• Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania
Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana.
Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.

Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.

Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.

Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.

🍅🍅Mazingira🌧️🌧️
• Hali ya Hewa:
Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.)

🍅🍅 Udongo:🌱🌱



Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.

🍅Aina za Nyanya🌱

Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)

Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
1. OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida
2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.

👉Kuandaa Kitalu cha Nyanya🍅

Mambo muhimu ya kuzingatia:
🎯 Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
🎯 Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
🎯 Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
🎯Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
🎯 Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.

🌱🌱Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya🍅

Aina ya matuta:
🌱🌱 matuta ya makingo (sunken seed bed)
🌱🌱 matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
🌱🌱 matuta ya kawaida (flat seed beds)

🎯Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta🎯
• Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].
• Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
• Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
• Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
• Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
• Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.

🎯🎯Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu🌱🌱



1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);
– matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
– Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
– Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.

Hasara:
o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri.

2. Matuta ya makingo (sunken seed beds):
Faida:
· matuta haya ni rahisi kutengeneza
· hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
· nyevu mdogo unaopatikana ardhini
· ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
· huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
· huzuia mmomonyoka wa ardhi

Hasara:
· Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
· mvua nyingi.

3. Matuta ya kawaida (flat seed beds):
Faida:
· ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
· na kusambazwa mbegu huoteshwa
· ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu

Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.

Kusia Mbegu
• Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
• Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
• Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
• Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
• Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.

Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight).
• Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
• Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini

Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni
• Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
• Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
• Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
• Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
• Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.

🌱🌱Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting
Rules)🌧️🌧️
🎯 Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
🎯Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
🎯Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
🎯 Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
🎯Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
🎯 Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
🎯Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
🎯 Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.

✍️✍️🍅Maandalizi ya Shamba
 la Nyanya📚📚



👉Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
👉Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
👉 Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
👉Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.

🌱🌱Jinsi ya kupanda miche:🍅


• Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
• Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
• Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
• Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani
• Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
• Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
• Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
• Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.
🍅🍅TUKUTANE SOKONI🍅🍅