Friday, April 24, 2020

KILIMO CHA VITUNGUU NA UTHIBITI WA MAGONJWA


Leo nimependa tujifunze kuhusiana na jinsi ya kukielekea kilimo cha Vitunguu maji.

Vitunguu ni moja ya zao la bustani linalopea na kutumiwa kwa wingi sana si hapa nchini tu bali duniani kote. Kitunguuu kinachukuwa nafasi ya pili baada ya nyanya. Kitunguu kinatumika katika kachumbari, kama kiungo kwenye kitoweo kama vile Samaki, nyama namboga za majani n.k.

 Majani ya vitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika kuandalia supu.

Aina Bora za Vitunguu Maji

1. NEPTUNE
Neptune
Hii ni mbegu bora zaidi ya kitunguu maji kwa sasa kwani hutoa mavuno mengi zaidi kuanzia tani 20 kwa hekari.
Kina rangi nzuri ya kupendeza
Huwa hakitoi mapacha katika yai la kitunguu.
Umbo lake ni kubwa na la duara.

2. Red Creole
download%2B%25283%2529
Hii ni mbegu bora pia katika zao la kitunguu.  Hutoa mavuno kuanzia tani 13 hadi 23 kwa ekari.

  • Kukomaa- siku 150
  • Shape- Nusu bapa
  • Rangi ya Ganda- Nyekundu
  • Ndani-Nyekundu kahawia

3. Red Bombay
images
Mavuno yake ni sawa na red Creole ila hutofautiana rangi na maisha rufani.
  •  siku-160
  • Shape -Duara
  • Rangi  ya ganda-Nyekundu angavu
  • Rangi ndani-Nyekundu kahawia
4. Texas Grano
images%2B%25282%2529
  • Kukomaa-165
  • Shape -Duara
  • Rangi ya ganda- Njano (kaki)
  • Rangi ndani -Nyeupe

HALI YA HEWA
Vitunguu hustawi maeneo yasiyo na mvua nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na maeneo yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa kwa vitunguu.

UDONGO
Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha, unaoruhusu mizizi kupenya na unaohifadhi unyevu kama vile udongo wa nusu mfinyanzi nusu tifutifu na wenye kiasi cha tindikali ya 5.5-6.5.

UPANDAJI WA MBEGU ZA VITUNGUU KWENYE KITALU.
Hapa kwetu Tanzania upandaji huanza mwezi March hadi Mei kutegemea na msimu wa kilimo ulivyo. Hivyo kilimo hiki huanza mara baada ya mvua kubwa za masika kumalizika. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vitunguu.
Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema katika kitalu. Mbegu zinaweza kutawanywa au kupandwa kwa mistari katika tuta la kitalu.Tengeneza matuta yenye upana wa mita 1 na urefu wowote kutegemea na mahitaji yako.Weka mbolea ya samadi ndoo moja hadi mbili kwa mraba wa mita moja.

Lima tuta kiasi cha sentimita 10-25.
Dnc7iTNUYAA5BTH
Sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 15 kutoka mstari hadi mstari Katika upandaji wa mstari mbegu hupandwa katika nafasi ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari. Gramu 5 (kijiko cha chai) zinatosha kusia eneo la mraba mita moja.
Tandaza nyasi na mwagilia.

Baada ya kupanda mbegu hufunikwa na udongo mwepesi na baadaye matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli miche michanga. Mbegu za vitunguu huota baada ya siku 7 hadi 10.

KIASI CHA MBEGU.
 Kilo 1.5 za mbegu zinatosha hekari moja ya shamba.

KUOMBEKA/KUPANDIKIZA MICHE BUSTANINI.

➡Upandikizaji wa miche ya vitunguu hufanyika baada ya miche kukua na kufikia unene wa Penseli. Mara nyingi miche hii hukaa kwenye kitalu kwa siku 35 -40 baada ya kupandwa.

Usichelewe kuhamishia miche kwani  miche mikubwa huanza kutoa maua badala ya kitunguu (bulbs). Hivyo mara nyingi miche ya namna hii hubaki na suke la maua tu.
Wakati wa kupandikiza usikate wala kupunguza majani. Miche ipandikizwe sm 30 kati ya mstari na mstari na sm 10 kati ya mche na mche.

Upandaji katika bustani hufanyika kwenye mistari katika matuta au kwenye vijaruba.
Vijaruba hutumika katika maeneo tambarare na yenye ukame ili kuhifadhi unyevu baada ya kumwagilia. Sehemu zenye udongo mzito na wenye maji mengi tumia matuta yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm 15 kutoka usawa wa ardhi.

➡KUMBUKA: Pandikiza miche wakati wa asubuhi au jioni na mwagilia maji ya kutosha kisha hakikisha maji hayatuami.

MBOLEA
Weka mbolea ya kukuzia katika wiki ya nne hadi sita baada ya kupandikiza.
Weka mbolea kwenye mstari na hakikisha isigusane na mimea. Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha wakati wa kuweka mbolea. Tumia UREA, CAN au SA.

UMWAGILIAJI
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) Umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba.

Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyo kua. Pia ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna. Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.

MATUMIZI YA MBOLEA.
Kwanza kabisa naomba niseme kuwa kuna kasumba ya watu wengi kuogopa matumizi ya mbolea za viwandani kwa dhwanna ya kwamba mbolea hizo zinaharibu udongo na ardhi kwa ujumla wake:

Kwa mimi niwatoe hofu juu ya hilo kwani si kweli kwamba matumizi ya mbolea za viwandani yanaharibu udongo bali ukweli ni kuwa matumizi mabaya na yasiyofuata utaratibu ya mbolea za viwandani yanaharibu udongo na ardhi kwa ujumla. Nitaandaa makala maalumu ya kujulisha umma ni jinsi gani matumizi ya mbolea hata zisizo za viwandani yanavyoweza kuharibu udongo na ardhi kwa ujumla wake.

Hapa tutaona juu ya makundi ya mbolea na muda/ kipindi cha matumizi  ya mbolea hizo.

1. MBOLEA KUNDI LA KWANZA.

Mbolea za kupandia.
Hizi huwekwa kabla au mara tu ya kuhamishia miche shambani. Mbolea hizi zina lengo la kusaidia ukuaji mzuri wa mifumo ya mzizi (root systems) itakayosaidia mmea kufyonza virutubisho na maji kutoka ktk udongo.

Mbolea hizi zina madini/ kirutubisho kikuu cha fosforasi (P), na huitwa mbolea za fosfeti (Phosphate Fertilizers), kundi hili lina mbolea kama MOP, TSP, DAP, Minjingu n.k.

2. MBOLEA ZA KUKUZIA
Mbolea hizi huwekwa kipindi cha ukuaji wa mmea (vegetative growth) na hua na lengo la kuupa mmea afya na ukuaji mzuri utakaopelekea kuwa na majani mazuri yatakayotengeneza chakula cha kutosha kwaajili ya mmea.
Kirutubisho kikuu katika kundi la mbolea hizi ni Nitrogen (N). Baadhi ya mbolea zilizopo kwenye kundi hili ni pamoja na UREA, SA, CAN n.k.

Pia kwenye kundi hili zipo mbolea za maji zinazopigwa kwenye majani (foliar fertilizers) hujulikana pia kama booster.

3. MBOLEA ZA KUZALISHA/KUKOMAZIA KITUNGU.
Hizi ni zile zinazowekwa kuusaidia mmea wa kitunguu  kutaga  (kutengeneza kitunguu). Mbolea hizi huwekwa mara tu kitunguu kinapoanza kutaga.

Kirutubisho kikuu ni ktk mbolea hizi Potassium. Ili Kituunguu kiweze kujijenga vizuri na kuwa na ubora kinahitaji mbolea zenye madini/ kirutubisho cha Potassium. Mfano wa mbolea zenye virutubisho hichi ni Multi K, MOP (Muriate of Potash) n.k.

INGIA HAPA KUONA MPANGILIO WA MBOLEA KATIKA ZAO LA KITUNGUU MAJI 

Zingatia kwamba ili mbolea ziweze kufanya kazi ni lazima uweke pindi ambapo kuna unyevu ktk udongo na uzingatie kumwagilia mara baada ya kuweka mbolea.
 EPUKA KUMWAGILIA MAJI MENGI KWANI VIRUTUBISHO HUENDA CHINI ZAIDI KTK UDONGO
Hayo ndio makundi makuu ya mbolea, japokua mbolea hizo hujumuisha pia virutubisho vidogo (micro nutrients) ambavyo vinahitajika kwa udogo kwenye mimea, japokua zina kazi muhimu kwenye mimea.

WADUDU WAHARIBIFU NA UDHIBITI WAKE KTK KILIMO CHA VITUNGUU

IFAHAMIKE: Ktk makala hii nimeainisha baadhi tu ya wadudu wasumbufu na namna/ njia chache za udhibiti wake. Pia nakaribisha mchango na namna nyengine juu ya udhibiti wa wadudu hawa.

UDHIBITI RAHISI WA MAGUGU 
katika shamba la kitunguu magugu hudhibitiwa kwa namna mbalimbali kama vile kung'olea, kwa jembe na kwa viuwa gugu.

Fahamu Dawa za kuuwa magugu vizuri zaidi shambani


USHAURI: Ni rahisi na gharama nyepesi zaidi kudhibiti magugu katika shamba la kitunguu kwa kutumia viuwa gugu kwa mda mchache.
TUMIA WILSTOP kudhibiti uotaji ama ukuaji wa magugu siku zisizo zidi tatu baada ya kupandikiza vitunguu shambani.
Hakikisha unatumia WILSTOP  majani ama magugu hayajaota ama kabla hajafikisha majani zaidi ya mawili.

Thiripi (Thrips):
images%2B%25283%2529
Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe. Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.

UDHIBITI
20181015_145250

Thrips huudhibitiwa kwa urahisi zaidi kwa kunyunyuzia dawa iitwayo Dudumectin au Duduwill.

Kimamba:
images%2B%252821%2529
Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.

KIDHIBITI

Wadudu hawa huthibitiwa kwa kunyunyuzia dawa iitwayo Dudumectin, willcron au Duduwill: zote hizi hufanya vizuri.

➡Sota (Cutworms):
images%2B%25284%2529
 Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao.

UDHIBITI
20181015_145230

Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama; Duduwill ambayo hutumika ndani ya wiki 0-7.
Duduwill hutumika kutibu udongo wenye wadudu kama hawa kwa kupulizia katika kitalu pia shambani huwadhibiti vizuri zaidi mara tu wanapooneka.

➡Utitiri wekundu (Red spider mites):
images%2B%252820%2529

Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.

KUDHIBITI
kupulizia dawa za wadudu Dudumectin huwadhibiti vizuri zaidi.

Vipekecha majani (leaf miner):
images%2B%252810%2529
Hawa ni aina ya inzi wadogo, ambao viwavi wake wanashambulia majani, kwa kupekecha na kutengeneza mitandao wa mitaro kwenye majani. Viwavi wanashambulia majani na kusababisha majani kukauka. Upungufu mkubwa wa mazao hutokea.

KUDHIBITI
kupulizia dawa ya wadudu kama Dudumectin au Duduwill .
kuteketeza masalia ya mazao
kutumia mzunguko wa mazao.

MAGONJWA NA UDHIBITI WAKE
Kitunguu ni zao amabalo haliwezi kustahimili magonjwa kwa hakika kama yalivyo baadhi ya mazao mengine, hivyo ni muhimu mkulima wa kitunguu ayafahamu magonjwa yote, dalili na namna ya udhibiti wake kabla hajaanza mradi wa kilimo cha kitunguu rasmi .

Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa sumbufu zaidi ktk vitunguu katika ukanda wa Afrika ya mashariki na Tanzania .

1.➡Baka zambarau (Puple Blotch).
pb

Ungonjwa huu unasababishwa na fangasi au Kuvu na
ugonjwa huu hujitokeza zaidi kipindi cha ukungu mwingi na unyevunyevu mwingi hasa wakati wa masika.

Zaidi ya 70 % ya mazao yanaweza kupotea kama ugonjwa hautadhibitiwa Haraka.

🔼DALILI
-madoa meupe yaliyodidimia huonekana kwenye majani na mashina ya kitunguu shambani.
-rangi ya zambarau kuwepo katikati ya doa jeupe.
-majani huanguka kuanzia juu

🔼UDHIBITI
20181031_174046


  • Panda mbegu safi na fanya kilimo cha mzunguko wa mazao.
  • Teketeza masalia ya kitunguu kilichokuwa na ugonjwa shambani kabla ya msimu mpya.
  • Pulizia dawa mfano  superwill (ya maji) au wilthane.
  • Pulizia dawa ya wilzeb kabla ugonjwa haujatokea.
  •  Kama kinga.


2.➡Kinyausi (Damping – off).
onion-downy-mildew-1L

Ugonjwa huu unasababishwa na fangasi na huenezwa kupitia udongo, mbegu na masalia ya mazao shambani.
Ugonjwa hujitokeza zaidi kitaluni panapokuwa na unyevunyevu mwingi au kuzidisha kiwango cha umwagiliaji hivyo udongo kuwa maji maji muda mrefu.

🔼DALILI
-mbegu huoza kabla hata ya kuota
-kunyauka kwa kiwango kikubwa cha miche ya kitunguu baada ya kuota

🔼Kudhibiti.
20181015_145603
  • Hakikisha mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya wilzeb au wilthane kabla ya kupanda.
  • Kusia mbegu kwa nafasi za kutosha
  • Kuepukana na kubananisha miche kitaluni
  •  Kuepukanana na kumwagilia maji wakati wa jua kali au wakati kuna ukungu
  • pulizia dawa ya super will inatibu na kukinga mmea dhidi magonjwa ya kuvu.


Virusi njano vya vitunguu (Onion yellow Dwarf virus)
ydv


-Ugonjwa huu unasababishwa na virusi na kuenezwa na wadudu aina ya vidukari (wadudu -mafuta).

🔼DALILI
  • Kujikunjakunja kwa majani kwa kutengeneza vinundu na uwepo wa mistari ya rangi ya manjano kwenye majani.
  • Hatimae mmea mzima kudumaa, kujikunja na kufa
🔼Kudhibiti:
  • tumia mbegu safi na bora iliyothibitishwa.
  • Kuweka shamba katika hali ya usafi muda wote
  • Kuzuia wadudu piga dawa inaitwa willcron profenofos au dudumectin kwa ufanyajikazi mzuri 
Ukungu mweusi
(Onion Black Mold)
images%2B%252811%2529

Kisababishi: Aspergillus niger

Ugonjwa huu maranyingi hutokea endapo joto litakua kali ktk mazingira.

🔼DALILI
  • Utando mweusi katika gamba la kitunguu.
  • Kuoza shingo na kirungu


🔼Kudhibiti:
-Hakikisha mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya  wilthane au super will kukinga na piga wilzeb au super will  kabla ya ugonjwa kutokea kama kinga na tiba pia.

3.➡Onion Botrytis leaf blight 
images%2B%252817%2529
Kisababishi : Botrytis allii

Ugonjwa huu huonekana wakati vitunguu vimehifadhiwa na maambukizi huanzia shambani.

DALILI
  • Kudumaa kwa kitunguu shambani
  • Sehemu zilizoathirika hukauka na kufa.
  • Gamba gumu katika shingo ya kitunguu huonekana
🔼TIBU
Tumia Wilthane kutibu ugonjwa huu.

4.➡Ubwiri unyoya
(Onion Downy Mildew)
images%2B%252819%2529

Kisababishi: Peronospora destructor
🔼DALILI
  • Kutokea kwa Madoa ya duara, rangi afifu ya njano kwenye majani makubwa na huenea  mpaka kwenye majani machanga.
  • katika majani majani makubwa, madoa ya njano hufunikwa na ukungu wa rangi ya kijivu.
  • Majani yaliyoathirika hulegea, kusinyaa na kukauka kuanzia kwenye ncha.
  • Hatimae Shina la mbegu huzungukwa na madonda na kusababisha kichwa cha mbegu kuanguka.
🔼Kudhibiti:
  • Safisha shamba ,Panda mbegu safi na zingatia kanuni za umwagiliaji
  • Tumia wilthane au super will kutibu pia wilzeb na super will hutumika kukinga.
Kutu (rust)
Leek%2BRust%2Bcrop%2B%25281%2529

Kisababishi: Puccinia porri

🔼DALILI
  • Majani yalioathirika huwa na madoa ya rangi ya machungwa
  • Baadaye hugeuka na kuwa meusi
  • Majani yaliyoathirika sana huwa ya njano na hatimaye hufa.
KUDHIBITI
  • Tumia super will au wilthane kutibu na kukinga ugonjwa huu.
MAVUNO NA MAUZO
Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganishwa na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri.
Hivi sasa bei ya chini kabisa ya vitunguu kilo moja ni Tsh 1000/= kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo. Ekari moja huvunwa Tani 13 hadi 23 sawa na kg 13,000 hadi 23,000. 
Kama mkulima ukipata soko la uhakika mkulima unaweza kupata hadi 13.5million  hadi  23 millions kwa msimu mmoja.

No comments:

Post a Comment