Friday, April 17, 2020

✍️Kilimo bora cha Mihogo✍️

🌱🌱Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani.

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO

👉👉Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Naliendele Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

🎯🎯Kiroba
Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Mbinu bora za kilimo cha muhogo

👉👉Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
- Kufyeka shamba
- Kung’a na kuchoma visiki
- Kulima na kutengeneza matuta
· Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.

🌱🌱· Upanadaji🌱🌱


Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
🎯- Kulaza ardhini (Horizontal)
🎯- Kusimamisha wima (Vertcal)
🎯- Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
 Inashauriwa urefu uwe cm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

👉👉Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

🎯🎯 Palizi:🎯🎯
✍️✍️- Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi minne ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindani wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
✍️✍️Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
✍️✍️Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
👉👉Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

🎯🎯Uvunaji:🛒🛒


👉👉Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

💰💰Usindikaji bora🌱🌱

Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
💗 kuharakisha ukaushaji
💗 Kuondoa sumu (cyanide) iliyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
💗 Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

🌱🌱Njia bora za usindikaji🛒🛒

👉👉 Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo.
👉👉 Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
- Kwa kutumia mashine aina ya chipper
- Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

👉👉Matumizi ya Muhogo🎯

✍️✍️Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
✍️✍️ Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
✍️✍️  Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga

KILIMO CHA KISASA CHA MATANGO

🥒🥒Kilimo bora Cha matango uboreshe kipato kwa muda mfupi
💰💰Hili ni zao la biashara, pia chakula. Zao hili hustawi na kulimwa kwa wingi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Pwani.

🥒🥒Matumizi: 🥒🥒
Matango hutumika kama tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo.

🌧️🌧️Hali ya hewa: ⛅⛅
Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi. Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.

🌈🌈Udongo:  🌈🌈
Kwa ustawi mzuri wa matango, udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita 1000-1200 kutoka usawa wa bahari.

🌱🌱Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.

🌱🌱Kupanda:🌱🌱
 Mara nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja, inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo.

🌱🌱Nafasi:🥒🥒


Nafasi kati ya mche na mche ni sentimita 60-70, na nafasi kati mstari na mstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwa iwekewe miti ili iweze kuzaa matunda mengi na kuepuka kukaa chini ambapo matunda yanaweza kuoza au kuharibiwa na wadudu.

💮💮Mbolea:🏵️🏵️
 Mbolea ni muhimu sana, kabla ya kupanda au kuhamisha miche. Mbolea inayoweza kutumika ni samadi au ya viwandani isiyokuwa na madhara kwa mazingira na afya ya binadamu. Baada ya kupanda, tumia mbolea ya maji maji kila baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda.

🎯🎯Palizi:🏵️🏵️
 Palizi ni muhimu , ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu.

Wadudu waharibifu: Wadudu waharibifu wa matango ni pamoja na Vidukari, inzi weupe, na minyoo ya mizizi.

🥒🥒Magonjwa: 🏵️🏵️
Magonjwa yaliyozoeleka kushambulia matango ni pamoja na Ukungu, fusari, na magonjwa ya virusi.

🛒🛒Kuvuna:🥒💰


Matango yanaweza kuwa tayari kuvunwa kuanzia siku 45-60 na matunda yanatakiwa yawe na urefu wa sentimita 15 mpaka 20. Makadirio ya mavuno ni tani 6 kwa ekari moja.
🛒🛒#TUKUTANE SOKONI💰💰

 🌱🌱 KILIMO AJIRA YANGU 💰

KILIMO BORA CHA MATIKITI MAJI

🍉Kilimo Bora cha Matikiti Maji mambo muhimu ya kufanya ili unufaike na KILIMO mapema zaidi.
✍️✍️UTANGULIZI🎯🍉
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.

🍉🍉Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.

🌱🌱HALI YA HEWA🌧️🌧️
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua : kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.

👉👉Hali ya Udongo🌧️🌧️
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

🍉🍉MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.🍉🍉
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa.

✍️UANDAAJI WA SHAMBA🍉

Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.

✍️✍️UPANDAJI🍉🍉
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)

✍️UPUNGUZAJI WA MIMEA🍉
Mimea ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.

Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.

🍉🍉Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.

🍉🍉Wakati mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.

👉MATANDAZO (MULCHES
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

✍️UWEKAJI WA MBOLEA✍️
Mbolea za viwandani aina ya NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana. Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.

🌧️🌧️UMWAGILIAJI🚿🚿
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.

🎯🎯Angalizo;
 usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.

🍉🍉MAUA NA MATUNDA🍉🍉
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k

🍉✍️Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.
Hii hufanywa kwa , kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.

👉MAGONJWA NA WADUDU

Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.

🎯🎯UVUNAJI MATIKITI🎯🎯






Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;

✍️🍉Rangi ya mng’ao hupotea
Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.
Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi

🛒🛒Soko la matikiti maji🛒🛒

Ukubwa wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja limekuwa likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti dogo mpaka 3000 kwa tikiti kubwa katika masoko.

🛒🛒Mavuno💰💰
Mavuno ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya TANI 15-36 kwa hekta moja.
🍉🍉TUKUTANE SOKONI🍉🍉
✍️🍉 KILIMO AJIRA YANGU 💰

KILIMO BORA CHA PAPAI

☘️☘️Kilimo bora Cha Papai🍁🍁
👉👉Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.

👉👉Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.

✍️Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu.✍️

🌱Mpapai wenye maua kiume tu.

🌱Mpapai wenye maua kike tu.

🌱Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya).

✍️✍️Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

✍️✍️Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.

🏵️UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.🏵️🏵️
Miche ya mpapai Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika:

1. Mbegu za Kawaida (Local seeds).
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote.

Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.

2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1 au MALAIKA F1.
UPANDAJI.

Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.

👉👉Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.

KITALU CHA MIPAPAI NA BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI.
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5. Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi. Kiasi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda.

Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yaliyoja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu. Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.

🌱🌱UANDAAJI WA SHAMBA.

👉👉Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba. Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.

👉👉Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.

Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekta (400 hadi 800 kwa ekari) Kupanda mimea shambani Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.

🌼UWEKAJI WA MBOLEA🌼
.
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbolea gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phosphate kwa kaisi kikubwa.

Mfano; - 12:24:12. (NPK) Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK) Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.

🌧️🌧️UMWAGILIAJI.⛅⛅
👉👉Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji ni ya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.

🌈🌈Magugu Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.

HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI.

🌱🌱Kitalu - Wiki 1 - 6 -Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa.

🌱🌱Shamba - wiki 7 -16 -Maua na kuweka matunda.

🌱🌱Wiki 17 - 21 -Kukua kwa matunda.

🌱🌱Wiki 22 - 26 -Mavuno ya kwanza

🎯🎯Wiki 37 -kuendelea Week 37 ni miezi tisa au kumi sio kwa hiyo kilimo cha mapapai huchukua miezi 10 kupata mavuno


💰💰GHARAMA 📝📝

🎯Kununua ekari moja inategemea na eneo ulipo na bei husika.
🎯Kununua mbegu tsh 50,000-100,000.
🎯Kumwagilizia kila siku
 🎯upandaji -kuhamisha kutoka kwenye vitalu hadi kwenye shamba -machine ya kumwagilizia 1,500,000/-
🎯Generator tsh lak 5
🎯Mbolea tsh 100,000 kila mwez -na vibarua shambani -kulima kwa trekta 40,000 Gharama zote kama mil 3-4 hiv mpaka kuvuna.

🌹🌹MAVUNO NA FAIDA.🛒🛒

💱💰Kama umelima ekarI moja unaweza ukapata matunda 15- 35 kwa mvuno wa Kwanza tu twende kimahesabu EkarI ina miche 400-800 Tuseme tupate miche 600 kwa ekari, kila mche utoe matunda 20 chini kabisa 600×20=12,000.
📚📚HIZI Ni hesabu Sio uchawi haya tuendelee kidogo.

🍐🍐Matunda Soko Kwa sasa unaweza ukauza kwa jumla jumla tsh 1500-3000 Tuuze kwa bei ya chini 1500 kwa kila papai 12000×1500=18,000,000/- Ukitoa Gharama za uendeshaji unaweza ukabaki na tsh 14,000,000 au toa 4,000,000 uweke kwenye dharura unaweza ukamake tsh 10 mil kwa ekar moja tu.
👉👉Nilikwambia Kilimo hesabu Sio uchawi
🛒🛒💰Mipesa iposhambani 🎯
🌱🌱Kilimo ajira yangu 🌱🌱

Wednesday, April 8, 2020

🐝BADILI MAISHA KWA UFUGAJI WA NYUKI

🌻🌻🌺 nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.

🌺🐝Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.

🌻🐝Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.

VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-

UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.

DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-

1. Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.

Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.

Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.

2. Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.

3. Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.

Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.

MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-

1. Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.

Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-

A. Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula. Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.

Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.

Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.

B. Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.

C. Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.

Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.

Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2. Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.

Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.

Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.

Monday, March 30, 2020

Sababu za kuku Kunyonyoka manyoya na njia za kumaliza tatizo



1. Kunyonyoka manyoya kwa kuku ni nini?
🐤🐤Ni mchakato wa asili na muhimu kwa kuku kupoteza/kujinyonyoa manyoya ya zamani yaliyovunjika ili kupata/kuota manyoya mapya.

🐥🦔 Kwa nini kuku wananyonyoka manyoya?🦔🦔

1️⃣• Sababu kuu ni kuku kumaliza mzunguko wake wa utagaji.

2️⃣Sababu ndogo ndogo ni👇👇
- Ukosefu wa chakula bora
- Ukosefu wa maji
- Joto kali sana
- Stress/ msongo wa kimwili, mfano majogoo kupanda jike moja mara nyingi.
🔔🔔NIWAKATI GANI KUKU HUNYONYOKA MANYOYA🐥

✍️✍️KUKU Katika ukuaji wao hunyonyoka manyoya mara 4 mpaka wanapokuwa wakubwa, na hivyo kupata manyoya kamili.
Vipindi hivyo ni wakiwa na umri wa wiki 1 - 6, wiki 7 - 9, wiki 12 - 13 na wiki 20 - 22.
🐓🐔🐓 Kuku wakubwa wananyonyoka manyoya angalau mara moja kwa mwaka. Na itamchukua kuku muda wa miezi 2 - 4 kumaliza mchakato wa kunyonyoka manyoya hadi kuota.

🐣🐣MATOKEO YA KUKU KUNYONYOKA MANYOYA HAYA HAPA.

🐓🐓• Kuku hupunguza kutaga au kuacha kabisa. Hii hutokana na kwamba 80-85% ya manyoya ni protein na 13% ya mayai ni protein, hivyo kuku hufanya uchaguzi wa kuitumia protein anayokula kwenye chakula katika ukuaji wa manyoya mapya na kupunguza protein kwenye kutengeneza mayai.

🐓🐓•Manyoya mengi kunyonyoka.
•Kuku wanaweza kuonekana kama wanaumwa na kupungua uzito.
🐓🐓•Kuku wanaweza kuwa wakorofi na wakali.
🐓🐓• Kuku wengine kwenye banda wanaweza kumdonoa ngozi kuku anayeota manyoya na kusababisha kutoka damu.

🐤🐤JINSI YA KUKABILINA NA TATIZO
LA KUNYONYOKA MANYOYA🐣🐣

•🐦🐦Walishe chakula chenye protein nyingi. Kwa kawaida chakula cha kuku wanaotaga huwa na protein 16%, kipindi cha kuku kunyonyoka manyoya ongeza protein ifike 20-25%.
🐦🐦•Hakikisha kuku wana chakula na maji muda wote.
🐦🐦• Hakikisha kuku hawasumbuliwi na kupata stress. Mfano, epuka kuleta kuku mgeni bandani,kelele.
🐦🐦•Epuka kuwabeba au kuwashika kuku kipindi hiki, kwani itawaumiza na kuwaongezea stress.
🐦🐦•Hakikisha kuku anayeota manyoya hadonolewi na wenzake.

🎯🎯#UFUGAJI AJILA YANGU🎯🎯

Sababu 10 Za Kuku Kupunguza Utagaji Mayai Na njia za kumaliza tatizo.


Sababu 10 Za Kuku Kupunguza Utagaji Mayai Na njia za kumaliza tatizo.🐣🐣🐣🐣

Kupungua kwa mayai yanayo zalishwa kwa siku katika shamba lako la kuku watagao mayai ni dalili moja wapo inayo onesha kwamba kunatatizo katika kundi lako la kuku. Kulingana na utafiti ulio fanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kwa kawaida kuku aliye fikia umri wa miezi mitano au sita nakuendelea inatakiwa atage yai moja kila baada ya saa 24 hadi 26, kwa maana hiyo kila siku kuku wako inatakiwa atage yai moja.

🐔Kama vile tunavyo kuwa makini kufuatilia kinyesi cha kuku kugundua kama kuku anaumwa au anatatizo vivyo hivyo tunapaswa kufuatilia uzalishaji wa mayai kwa siku. Mabadiliko katika uzalishaji wa mayai yanaweza kusababishwa na magonjwa, mabadiliko ya tabia, mazingira na stress. Ilikujua sababu haswa inayo badilisha uzalishaji wa mayai katika kundi lako la kuku (flock) ina takiwa urejee na ukague historia ya kundi lako na pia ukague hali ya kuku wote(physical assessment) huku ukijiuliza maswali yafutayo;-

·   🐓Je kuna kuku wapya au wageni umewaongeza kwenye kundi lako?, kwasababu kuku wageni huweza kuwa chanzo cha kuleta magonjwa kama sehemu walio toka kuna mlipuko wa ugonjwa.
     
 🐓🐓Baada ya kujiuliza maswali kama hayo mara nyingi kisababishi haswaa cha tatizo hili hujulikana, zifuatazo ni sababu kumi zinazo weza kusababisha uzalishaji wa mayai kushuka katika kundi lako la kuku wa mayai.

1. KUPUNGUA KWA MASAA YA MWANGA (LIGHTING).

Mwanga husisimua “ pituitary gland”kwenye kuku ili kuchochea uzalishaji wa mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa mayai kwa kuku huhitaji masaa 14 mpaka 16 ya mwanga, kwa mfano kuna baadhi ya majira ya mwaka ambapo jua huwahi kuzama na kuchelewa kuchomoza hivyo husababisha masaa ya mwanga kuwa machache kwa siku, hivyo huathili uzalishaji wa mayai kwa kuku.

🐣🐣Ili kuondoa tatizo hili la upungufu wa masaa ya mwanga unaweza kuweka taa za umeme(artificial light) ndani ya banda lako la kuku wa mayai na uziwashe baada tu ya giza kuingia kwa masaa mawili hadi matatu. Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kuwapa kuku wako mwanga kwa msaa mawili hadi matatu huweza kuimalisha utagaji wa mayai kwa asilimia 20 hadi 30, hii inaonesha ni jinsi gani mwanga ni muhimu sana kwa kuku wa mayai.

2. STRESS NA MABADILIKO MBALIMBALI.
🐣🐤Ni rahisi sana kwa kuku kuathirika na stress na hii hupelekea kupunguza utagaji wa mayai, kwa kawaida kuku hapendi mabadiliko, yanaweza kuwa mabadiliko ya chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji ndani ya banda na kuwa hamisha kwenda banda jingine, pia stress inaweza sababishwa mambo kama kusumbuliwa na minyoo, kupe, viroboto, na chawa, joto kari, kelele za wanyama kama mbwa au paka, kelele za machine au magari zisizo isha, yote hayo yanaweza sababisha stress kwa kuku na hatimaye kuathili utagaji wa mayai.

3. MAGONJWA.
🐓🐣Kuku anapo shambuliwa na magonjwa mara nyingi hudhoofu na kukosa nguvu mwilini pia hupoteza hamu ya kula, katika wkati kama huu kuku hupunguza utagaji au kusismisha kabisa utagaji kutegemeana na namna ugonjwa ulivyo muathili. Kuepuka matatizo haya hakikisha kwamnba kuku wanapewa chanzo zote wanazo stahili, watibu kwa wakati pale wanapo ugua na pia jitahidi sana kuzuia vyanzo vya magonjwa ambavyo vipo ndani uwezo wako kama mfugaji.

4. UMRI WA KUKU
🐣🐓Kwa kawaida kuku anapo fikisha umri wa miaka miwili uzalishaji wake wa mayai hupungua, jinsi anavyo zidi kuwa na umri mkubwa uzalishaji wa mayai hupungua lakini huwa wanataga mayai makubwa kiumbo kuliko kuku wadogo. Ili kuongeza faida na ufanishi katika mradi wako hakikisha kwamba unaondoa kuku walio zeka na kuwaleta wengine ambao hawajazeka, kwasababu hao kuku wazee wanaweza wakawa wanakula chakula kingi lakini hawatagi hivyo husababisha hasara ndani ya shamba.

5. UKOSEFU WA MAJI
🐣🐓Upatikanaji wa maji safi na salama ni wa muhimu sana katika mfumo wa kutengeneza mayai kwa kuku. Uzalisha wa mayai huathirika endapo kuku wako hawatakunywa maji ya kutosha pengine kwa sababu ni machafu, hayajawekwa mahala ambapo panafikika vizuri hivyo kuku wanashindwa kunywa kiurahisi au hayana radha halisi ya maji kutokana uchafu au vitu ambavyo vimechanganywa ndani yake. Hakikisha kwamba maji safi na salma yanapatikana ndani ya banda muda wote na yaweke mahali ambapo panafikika na pia hakikisha kwamba idadi ya vyombo vya maji ina kidhi mahitaji kulingana na idadi ya kuku wako.

6. JOTO (TEMPERATURE).
🐣🐓Mtiririko wa utagaji wa mayai kwa kuku waweza athiriwa na joto katika mazingira husika. Kwa kawaida ili kuku aendele kutaga katika mtiririko wake  wa kawaida yani yai moja kila siku anahitaji joto lisiwe chini ya 11 oC na lisiwe zaidi 28 oc .

7. MATATIZO KATIKA MFUMO WA UZAZI
🐓🐣Magojwa au kasoro za kimaumbile katika mfumo wa uzazi pia zaweza sababisha kushuka kwa utagaji wa mayai, kwahiyo hakikisha kwamba kuku wako wa mayai hana matatizo ya kimaumbile. Tafuta msaada wa dakitari wa mifugo kama kuku ata onekana kuwa amevimba au ametuna kama mfano wa puto lenye maji upande wa chini wa tumbo au unaweza ona kama kuna dalili ya yai kukwama .

8. UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO.
🐓🐤Upungufu wa virutubisho muhimu katika chakula cha kuku wa mayai husababish kuaungua kwa uzalishaji wa mayai. Hakikisha kwamba kuku wako wanapewa chakula ambacho kina virutubisho vyote ambavyo ni vya muhimu kwake. Ili kuondoa tatizo hili unaweza kununua chakula kutoka madukani ambacho kimeshafanyiwa mchanganyiko maalumu wa virutubisho vinavyo faa kwa kuku wa mayai au ilikupunguza ghalama unaweza kujifunza fomula mbalimbali za mchanganyiko wa chakula na ukatengeneza chakula chako mwenyewe kwajili ya kuku wako. Katika chakula hicho cha kukuk wa mayai hakikisha kwamba kuna kiwango cha kutosha cha protini, madini kashiamu na wanga.

9. KUPUKUTISHA MANYOYA (MOLTING).🐓
🐣🐓Hii ni tabia ya asili ambayo hutokea kwa kuku katika hatua mbailimbali ya ukuaji, baadhi ya kuku wanaweza kupukutisha manyoya mengi kwa wakati mmoja na akabaki wazi baadhi ya sehemu za mwili wake kama mgongo na shingo au akapukutisha manyoya yake kidokidogo huku mengine yakiota, ambapo haitakuwa rahisi kwa wewe kugundua kama yupo katika hatua hii ya kupukutisha manyoya
🐔Katika kipindi hiki kuku hupunguza au kusimamisha kabisa utagaji, hii hutokana na ukweli kwamba kipindi hiki kuku hutumia protini nyingi na nguvu nyingi kuotesha manyoya mapya mwilini mwake kuliko kuzalisha mayai. Hali hii ni ya asili na haizuiliki kinacho takiwa katika kipindi hiki ni kujitahidi kumpa chakula ambacho ni bora(balanced diet).

10. HALI YA KUATAMIA.
🐣🐓Hi ni hali ya kuku kulalia mayai yake ili kuyapa joto na kuruhusu ukuaji wa kiini tete (embryo) ndani ya yai. Hali hii ni kawaida kwa kuku wetu wa asili. Kuku anapo anza kuatamia huacha kutaga mayai, pia kama kuku huyu anaye atamia yupo ndani ya banda ambalo kuku wengine bado wanaendelea kutaga, hupelekea kuku wengine kupatwa na hali hii pale tu wanapo muona ka atamia. Kwahiyo ni vyema kuku wanao atamia wasikae kweny banda moja na wale wanao endelea kutaga.

🐤ZINGATIA HAYA ILI KUONGEZA KIPATO CHAKO ,UKIONA SHIDA BADO MUONE MTAARAMU WA MIFUGO
🐓🐓🐓