Monday, March 30, 2020

Sababu za kuku Kunyonyoka manyoya na njia za kumaliza tatizo



1. Kunyonyoka manyoya kwa kuku ni nini?
🐀🐀Ni mchakato wa asili na muhimu kwa kuku kupoteza/kujinyonyoa manyoya ya zamani yaliyovunjika ili kupata/kuota manyoya mapya.

πŸ₯πŸ¦” Kwa nini kuku wananyonyoka manyoya?πŸ¦”πŸ¦”

1️⃣• Sababu kuu ni kuku kumaliza mzunguko wake wa utagaji.

2️⃣Sababu ndogo ndogo niπŸ‘‡πŸ‘‡
- Ukosefu wa chakula bora
- Ukosefu wa maji
- Joto kali sana
- Stress/ msongo wa kimwili, mfano majogoo kupanda jike moja mara nyingi.
πŸ””πŸ””NIWAKATI GANI KUKU HUNYONYOKA MANYOYAπŸ₯

✍️✍️KUKU Katika ukuaji wao hunyonyoka manyoya mara 4 mpaka wanapokuwa wakubwa, na hivyo kupata manyoya kamili.
Vipindi hivyo ni wakiwa na umri wa wiki 1 - 6, wiki 7 - 9, wiki 12 - 13 na wiki 20 - 22.
πŸ“πŸ”πŸ“ Kuku wakubwa wananyonyoka manyoya angalau mara moja kwa mwaka. Na itamchukua kuku muda wa miezi 2 - 4 kumaliza mchakato wa kunyonyoka manyoya hadi kuota.

🐣🐣MATOKEO YA KUKU KUNYONYOKA MANYOYA HAYA HAPA.

πŸ“πŸ“• Kuku hupunguza kutaga au kuacha kabisa. Hii hutokana na kwamba 80-85% ya manyoya ni protein na 13% ya mayai ni protein, hivyo kuku hufanya uchaguzi wa kuitumia protein anayokula kwenye chakula katika ukuaji wa manyoya mapya na kupunguza protein kwenye kutengeneza mayai.

πŸ“πŸ“•Manyoya mengi kunyonyoka.
•Kuku wanaweza kuonekana kama wanaumwa na kupungua uzito.
πŸ“πŸ“•Kuku wanaweza kuwa wakorofi na wakali.
πŸ“πŸ“• Kuku wengine kwenye banda wanaweza kumdonoa ngozi kuku anayeota manyoya na kusababisha kutoka damu.

🐀🐀JINSI YA KUKABILINA NA TATIZO
LA KUNYONYOKA MANYOYA🐣🐣

•πŸ¦πŸ¦Walishe chakula chenye protein nyingi. Kwa kawaida chakula cha kuku wanaotaga huwa na protein 16%, kipindi cha kuku kunyonyoka manyoya ongeza protein ifike 20-25%.
🐦🐦•Hakikisha kuku wana chakula na maji muda wote.
🐦🐦• Hakikisha kuku hawasumbuliwi na kupata stress. Mfano, epuka kuleta kuku mgeni bandani,kelele.
🐦🐦•Epuka kuwabeba au kuwashika kuku kipindi hiki, kwani itawaumiza na kuwaongezea stress.
🐦🐦•Hakikisha kuku anayeota manyoya hadonolewi na wenzake.

🎯🎯#UFUGAJI AJILA YANGU🎯🎯

No comments:

Post a Comment