Monday, March 30, 2020

Sababu za kuku Kunyonyoka manyoya na njia za kumaliza tatizo



1. Kunyonyoka manyoya kwa kuku ni nini?
๐Ÿค๐ŸคNi mchakato wa asili na muhimu kwa kuku kupoteza/kujinyonyoa manyoya ya zamani yaliyovunjika ili kupata/kuota manyoya mapya.

๐Ÿฅ๐Ÿฆ” Kwa nini kuku wananyonyoka manyoya?๐Ÿฆ”๐Ÿฆ”

1️⃣• Sababu kuu ni kuku kumaliza mzunguko wake wa utagaji.

2️⃣Sababu ndogo ndogo ni๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
- Ukosefu wa chakula bora
- Ukosefu wa maji
- Joto kali sana
- Stress/ msongo wa kimwili, mfano majogoo kupanda jike moja mara nyingi.
๐Ÿ””๐Ÿ””NIWAKATI GANI KUKU HUNYONYOKA MANYOYA๐Ÿฅ

✍️✍️KUKU Katika ukuaji wao hunyonyoka manyoya mara 4 mpaka wanapokuwa wakubwa, na hivyo kupata manyoya kamili.
Vipindi hivyo ni wakiwa na umri wa wiki 1 - 6, wiki 7 - 9, wiki 12 - 13 na wiki 20 - 22.
๐Ÿ“๐Ÿ”๐Ÿ“ Kuku wakubwa wananyonyoka manyoya angalau mara moja kwa mwaka. Na itamchukua kuku muda wa miezi 2 - 4 kumaliza mchakato wa kunyonyoka manyoya hadi kuota.

๐Ÿฃ๐ŸฃMATOKEO YA KUKU KUNYONYOKA MANYOYA HAYA HAPA.

๐Ÿ“๐Ÿ“• Kuku hupunguza kutaga au kuacha kabisa. Hii hutokana na kwamba 80-85% ya manyoya ni protein na 13% ya mayai ni protein, hivyo kuku hufanya uchaguzi wa kuitumia protein anayokula kwenye chakula katika ukuaji wa manyoya mapya na kupunguza protein kwenye kutengeneza mayai.

๐Ÿ“๐Ÿ“•Manyoya mengi kunyonyoka.
•Kuku wanaweza kuonekana kama wanaumwa na kupungua uzito.
๐Ÿ“๐Ÿ“•Kuku wanaweza kuwa wakorofi na wakali.
๐Ÿ“๐Ÿ“• Kuku wengine kwenye banda wanaweza kumdonoa ngozi kuku anayeota manyoya na kusababisha kutoka damu.

๐Ÿค๐ŸคJINSI YA KUKABILINA NA TATIZO
LA KUNYONYOKA MANYOYA๐Ÿฃ๐Ÿฃ

•๐Ÿฆ๐ŸฆWalishe chakula chenye protein nyingi. Kwa kawaida chakula cha kuku wanaotaga huwa na protein 16%, kipindi cha kuku kunyonyoka manyoya ongeza protein ifike 20-25%.
๐Ÿฆ๐Ÿฆ•Hakikisha kuku wana chakula na maji muda wote.
๐Ÿฆ๐Ÿฆ• Hakikisha kuku hawasumbuliwi na kupata stress. Mfano, epuka kuleta kuku mgeni bandani,kelele.
๐Ÿฆ๐Ÿฆ•Epuka kuwabeba au kuwashika kuku kipindi hiki, kwani itawaumiza na kuwaongezea stress.
๐Ÿฆ๐Ÿฆ•Hakikisha kuku anayeota manyoya hadonolewi na wenzake.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏ#UFUGAJI AJILA YANGU๐ŸŽฏ๐ŸŽฏ

Sababu 10 Za Kuku Kupunguza Utagaji Mayai Na njia za kumaliza tatizo.


Sababu 10 Za Kuku Kupunguza Utagaji Mayai Na njia za kumaliza tatizo.๐Ÿฃ๐Ÿฃ๐Ÿฃ๐Ÿฃ

Kupungua kwa mayai yanayo zalishwa kwa siku katika shamba lako la kuku watagao mayai ni dalili moja wapo inayo onesha kwamba kunatatizo katika kundi lako la kuku. Kulingana na utafiti ulio fanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kwa kawaida kuku aliye fikia umri wa miezi mitano au sita nakuendelea inatakiwa atage yai moja kila baada ya saa 24 hadi 26, kwa maana hiyo kila siku kuku wako inatakiwa atage yai moja.

๐Ÿ”Kama vile tunavyo kuwa makini kufuatilia kinyesi cha kuku kugundua kama kuku anaumwa au anatatizo vivyo hivyo tunapaswa kufuatilia uzalishaji wa mayai kwa siku. Mabadiliko katika uzalishaji wa mayai yanaweza kusababishwa na magonjwa, mabadiliko ya tabia, mazingira na stress. Ilikujua sababu haswa inayo badilisha uzalishaji wa mayai katika kundi lako la kuku (flock) ina takiwa urejee na ukague historia ya kundi lako na pia ukague hali ya kuku wote(physical assessment) huku ukijiuliza maswali yafutayo;-

·   ๐Ÿ“Je kuna kuku wapya au wageni umewaongeza kwenye kundi lako?, kwasababu kuku wageni huweza kuwa chanzo cha kuleta magonjwa kama sehemu walio toka kuna mlipuko wa ugonjwa.
     
 ๐Ÿ“๐Ÿ“Baada ya kujiuliza maswali kama hayo mara nyingi kisababishi haswaa cha tatizo hili hujulikana, zifuatazo ni sababu kumi zinazo weza kusababisha uzalishaji wa mayai kushuka katika kundi lako la kuku wa mayai.

1. KUPUNGUA KWA MASAA YA MWANGA (LIGHTING).

Mwanga husisimua “ pituitary gland”kwenye kuku ili kuchochea uzalishaji wa mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa mayai kwa kuku huhitaji masaa 14 mpaka 16 ya mwanga, kwa mfano kuna baadhi ya majira ya mwaka ambapo jua huwahi kuzama na kuchelewa kuchomoza hivyo husababisha masaa ya mwanga kuwa machache kwa siku, hivyo huathili uzalishaji wa mayai kwa kuku.

๐Ÿฃ๐ŸฃIli kuondoa tatizo hili la upungufu wa masaa ya mwanga unaweza kuweka taa za umeme(artificial light) ndani ya banda lako la kuku wa mayai na uziwashe baada tu ya giza kuingia kwa masaa mawili hadi matatu. Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kuwapa kuku wako mwanga kwa msaa mawili hadi matatu huweza kuimalisha utagaji wa mayai kwa asilimia 20 hadi 30, hii inaonesha ni jinsi gani mwanga ni muhimu sana kwa kuku wa mayai.

2. STRESS NA MABADILIKO MBALIMBALI.
๐Ÿฃ๐ŸคNi rahisi sana kwa kuku kuathirika na stress na hii hupelekea kupunguza utagaji wa mayai, kwa kawaida kuku hapendi mabadiliko, yanaweza kuwa mabadiliko ya chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji ndani ya banda na kuwa hamisha kwenda banda jingine, pia stress inaweza sababishwa mambo kama kusumbuliwa na minyoo, kupe, viroboto, na chawa, joto kari, kelele za wanyama kama mbwa au paka, kelele za machine au magari zisizo isha, yote hayo yanaweza sababisha stress kwa kuku na hatimaye kuathili utagaji wa mayai.

3. MAGONJWA.
๐Ÿ“๐ŸฃKuku anapo shambuliwa na magonjwa mara nyingi hudhoofu na kukosa nguvu mwilini pia hupoteza hamu ya kula, katika wkati kama huu kuku hupunguza utagaji au kusismisha kabisa utagaji kutegemeana na namna ugonjwa ulivyo muathili. Kuepuka matatizo haya hakikisha kwamnba kuku wanapewa chanzo zote wanazo stahili, watibu kwa wakati pale wanapo ugua na pia jitahidi sana kuzuia vyanzo vya magonjwa ambavyo vipo ndani uwezo wako kama mfugaji.

4. UMRI WA KUKU
๐Ÿฃ๐Ÿ“Kwa kawaida kuku anapo fikisha umri wa miaka miwili uzalishaji wake wa mayai hupungua, jinsi anavyo zidi kuwa na umri mkubwa uzalishaji wa mayai hupungua lakini huwa wanataga mayai makubwa kiumbo kuliko kuku wadogo. Ili kuongeza faida na ufanishi katika mradi wako hakikisha kwamba unaondoa kuku walio zeka na kuwaleta wengine ambao hawajazeka, kwasababu hao kuku wazee wanaweza wakawa wanakula chakula kingi lakini hawatagi hivyo husababisha hasara ndani ya shamba.

5. UKOSEFU WA MAJI
๐Ÿฃ๐Ÿ“Upatikanaji wa maji safi na salama ni wa muhimu sana katika mfumo wa kutengeneza mayai kwa kuku. Uzalisha wa mayai huathirika endapo kuku wako hawatakunywa maji ya kutosha pengine kwa sababu ni machafu, hayajawekwa mahala ambapo panafikika vizuri hivyo kuku wanashindwa kunywa kiurahisi au hayana radha halisi ya maji kutokana uchafu au vitu ambavyo vimechanganywa ndani yake. Hakikisha kwamba maji safi na salma yanapatikana ndani ya banda muda wote na yaweke mahali ambapo panafikika na pia hakikisha kwamba idadi ya vyombo vya maji ina kidhi mahitaji kulingana na idadi ya kuku wako.

6. JOTO (TEMPERATURE).
๐Ÿฃ๐Ÿ“Mtiririko wa utagaji wa mayai kwa kuku waweza athiriwa na joto katika mazingira husika. Kwa kawaida ili kuku aendele kutaga katika mtiririko wake  wa kawaida yani yai moja kila siku anahitaji joto lisiwe chini ya 11 oC na lisiwe zaidi 28 oc .

7. MATATIZO KATIKA MFUMO WA UZAZI
๐Ÿ“๐ŸฃMagojwa au kasoro za kimaumbile katika mfumo wa uzazi pia zaweza sababisha kushuka kwa utagaji wa mayai, kwahiyo hakikisha kwamba kuku wako wa mayai hana matatizo ya kimaumbile. Tafuta msaada wa dakitari wa mifugo kama kuku ata onekana kuwa amevimba au ametuna kama mfano wa puto lenye maji upande wa chini wa tumbo au unaweza ona kama kuna dalili ya yai kukwama .

8. UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO.
๐Ÿ“๐ŸคUpungufu wa virutubisho muhimu katika chakula cha kuku wa mayai husababish kuaungua kwa uzalishaji wa mayai. Hakikisha kwamba kuku wako wanapewa chakula ambacho kina virutubisho vyote ambavyo ni vya muhimu kwake. Ili kuondoa tatizo hili unaweza kununua chakula kutoka madukani ambacho kimeshafanyiwa mchanganyiko maalumu wa virutubisho vinavyo faa kwa kuku wa mayai au ilikupunguza ghalama unaweza kujifunza fomula mbalimbali za mchanganyiko wa chakula na ukatengeneza chakula chako mwenyewe kwajili ya kuku wako. Katika chakula hicho cha kukuk wa mayai hakikisha kwamba kuna kiwango cha kutosha cha protini, madini kashiamu na wanga.

9. KUPUKUTISHA MANYOYA (MOLTING).๐Ÿ“
๐Ÿฃ๐Ÿ“Hii ni tabia ya asili ambayo hutokea kwa kuku katika hatua mbailimbali ya ukuaji, baadhi ya kuku wanaweza kupukutisha manyoya mengi kwa wakati mmoja na akabaki wazi baadhi ya sehemu za mwili wake kama mgongo na shingo au akapukutisha manyoya yake kidokidogo huku mengine yakiota, ambapo haitakuwa rahisi kwa wewe kugundua kama yupo katika hatua hii ya kupukutisha manyoya
๐Ÿ”Katika kipindi hiki kuku hupunguza au kusimamisha kabisa utagaji, hii hutokana na ukweli kwamba kipindi hiki kuku hutumia protini nyingi na nguvu nyingi kuotesha manyoya mapya mwilini mwake kuliko kuzalisha mayai. Hali hii ni ya asili na haizuiliki kinacho takiwa katika kipindi hiki ni kujitahidi kumpa chakula ambacho ni bora(balanced diet).

10. HALI YA KUATAMIA.
๐Ÿฃ๐Ÿ“Hi ni hali ya kuku kulalia mayai yake ili kuyapa joto na kuruhusu ukuaji wa kiini tete (embryo) ndani ya yai. Hali hii ni kawaida kwa kuku wetu wa asili. Kuku anapo anza kuatamia huacha kutaga mayai, pia kama kuku huyu anaye atamia yupo ndani ya banda ambalo kuku wengine bado wanaendelea kutaga, hupelekea kuku wengine kupatwa na hali hii pale tu wanapo muona ka atamia. Kwahiyo ni vyema kuku wanao atamia wasikae kweny banda moja na wale wanao endelea kutaga.

๐ŸคZINGATIA HAYA ILI KUONGEZA KIPATO CHAKO ,UKIONA SHIDA BADO MUONE MTAARAMU WA MIFUGO
๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“

Sunday, March 29, 2020

Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa Gumboro na njisi ya kukika kuku

Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa Gumboro ( Infectious

Bursal Diseases) unaowasumBa wafugaji wa kuku.

Ni ugonjwa wa  utokanao na virusi  viitwavyo ”BIRNAVIRUS" . Ugonjwa huu huwashambulia kuku na ndege wengine wafugwao. 
i.Kuenea/kusambaa kwa ugonjwa.
ii.Kutoka banda moja kwenda linginge.
iii.Kupitia kinyesi kinyesi cha kuku anayeumwa.

๐ŸŽฏ๐ŸŽฏDaa Ugonjwa
✍️Kuku hutapika na kuharisha majimaji.

✍️Manyoya husimama.

✍️Kuku husinzia na kukosa hamu ya kula.

✍️Vifo hufikia hadi asilimia thelathini (30%).

✍️Kuujidokoadokoa sehemu ya haja kubwa.

✍️Cha ngozi hasa mapajani vidonda hutokea hasa vifaranga.

๐Ÿ™Jinsi  ya kukinga na kuzuia ugonjwa wa Gumboro
Safisha banda kwa dawa za kuua vijidudu (Disinfectants).

Wapatie chanjo ya Gumboro vifaranga wakiwa na umri wa wiki 2 na rudia tena wakiwa na umri wa wiki 3 (yaan siku ya 14 na 21)

Tiba za ugonjwa wa Gumboro
Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada zaidi wasiliana na mtaalam au daktari wa mifugo. Asante
๐Ÿ””๐Ÿ””UFUGAJI AJIRA YANGU

Saturday, March 28, 2020

๐Ÿ” KANUNI ZA UTOAJI WA CHANJO NA KINGA MUHIMU KWA KUKU WA MAYAI, CHOTARA NA KIENYEJI

๐Ÿ” KANUNI ZA UTOAJI WA CHANJO  KWA KUKU WA MAYAI, CHOTARA NA KIENYEJI
https://play.google.com/store/apps/details?id=mwanaapp.appjbh:

๐ŸฅSIKU 1.
 Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus.

๐ŸฅSIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kisha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa vitamini.

๐ŸฅSIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu.

๐ŸฅSiku ya 21 (wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri)

๐ŸฅSIKU 28 (Mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD

๐ŸฅSIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.

๐ŸฅWIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.

๐ŸฅWIKI YA 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle.
#Asante,#ufugaji Ajira yangu

☑️☑️Cha msingi wewe bonyeza link ya MwanaApp ili uweze kujifunza #UFUGAJI NA KILIMO BORA mkononi mwako ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡https://play.google.com/store/apps/details?id=mwanaapp.appjbh

Thursday, March 26, 2020

SIFA ZA NG'OMBE BORA WA MAZIWA๐ŸŒน

✍️ SIFA ZA NG’OMBE WA MAZIWA

๐Ÿ„๐ŸฎUmbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani

๐Ÿ„ ๐ŸฎMgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani

๐Ÿ„ ๐ŸฎMiguu mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara

๐Ÿ„๐ŸฎKiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu, na unene wa wastani

๐Ÿ„๐ŸฎNafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha

๐Ÿ„๐ŸฎEndapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa

๐Ÿฎ๐Ÿฎ Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, Jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchanganyiko wa aina hizo na Zebu.

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ

Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe:
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2-3 za maziwa anayotoa,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Apewe madini na virutubisho vingine kulingana na mahitaji,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Baada ya kusitisha kukamuliwa, apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa;
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
๐Ÿ“๐Ÿ“ MwanaApp ๐Ÿ”๐Ÿ”

UGONJWA WA NDUI YA KUKU NA TIBA YAKE

๐Ÿ”๐Ÿ“ŒNAMNA YA KUTIBU UGONJWA WA NDUI YA KUKU KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI.


DALILI ZA UGONJWA WA NDUI.
· Uonjwa wa ndui utaona kuku wako wamepata mapele kwenye kichwa yenye rangi ya kahawia, mapele hayo yanaweza kuziba mpaka macho kufanya kuku wako wasione kabisa na kusababisha kuku wako wakashindwa kula hivyo wakadhoofika kabisa na hatimaye kufa. Ugonjwa huu huwapata kuku wa rika zote lakini huathiri sana vifaranga.


Mara nyingi magonjwa ya virusi ni magonjwa ambayo hayana tiba lakini yana kinga. Wachanje kuku wako hasa vifarnga wanapokua wamefikia umri wa siku 56yani wiki nane(8), na kama usipowachanja kuku wako na kwa bahati mbaya ugonjwa huu ukaingia bandani kwako basi la kufanya ni hili hapa..
NAMNA YA KUTIBU UGONJWA WA NDUI.
Njia hii nimeshaitumia mara kadhaa pale ugonjwa ulipowapata kuku wangu na ikanipa matokeo chanya kwa asilimia 95%.
Kwana kabisa nunua OTC 20% pamoja na vitamin, wachanganyie kuku wako kwenye maji ili kuwaepusha na magonjwa nyemelezi kwa sababu wanpokua wanashambuliwa na ugonjwa wa ndui ugonjwa wa ndui una sifa ya kupunguza sana kinga ya mwili, kinga ya mwili kwa kuku wako inashuka sana hivyo inakua rahihisi kwa kuku wako kuambukizwa magonjwa mengine, kwa hiyo unapokua unawapatia OTC 20% pamoja na VITAMINinawasaidia kuboost kinga ya mwili..
Sasa uatafanyaje ili kutibu ugonjwa wa ndui? Kwanza kabisa tafuta mafuta ya ng’ombe yanapatikana masokoni hasa masoko makubwa makubwa unaweza ukanunua maziwa freshi ambayo hayajawekewa maji ukayagandisha alafu ile samli ya juu ukaichukua kama mafuta ya ng’ombe.

Unayafanyaje sasa hayo mafuta ya ngo’mbe, Mafuta hayo unawapakaa kuku wako maeneo ambayo yana hayo madonda. Unapaka mara mbili kwa siku asubuhi na jioni ndani ya siku mbili. Baadae yale madonda yanakua yamelainila na unaweza kuyabandua bila shida yoyota na kuku wako wanakua vizuri na wanakua wamepona.
kama kuna njia nyingine unayoitumia kutibu ugonjwa huu basi usisite kushare na wengine kwa kucoment hapo juu palipoanfikwa answer. Ahsante, kwa pamoja tunajenga uchumi.