Thursday, March 26, 2020

SIFA ZA NG'OMBE BORA WA MAZIWA๐ŸŒน

✍️ SIFA ZA NG’OMBE WA MAZIWA

๐Ÿ„๐ŸฎUmbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani

๐Ÿ„ ๐ŸฎMgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani

๐Ÿ„ ๐ŸฎMiguu mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara

๐Ÿ„๐ŸฎKiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu, na unene wa wastani

๐Ÿ„๐ŸฎNafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha

๐Ÿ„๐ŸฎEndapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa

๐Ÿฎ๐Ÿฎ Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, Jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchanganyiko wa aina hizo na Zebu.

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ

Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe:
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2-3 za maziwa anayotoa,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Apewe madini na virutubisho vingine kulingana na mahitaji,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe,
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Baada ya kusitisha kukamuliwa, apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa;
๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
๐Ÿ“๐Ÿ“ MwanaApp ๐Ÿ”๐Ÿ”

No comments:

Post a Comment